• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Maafisa Elimu kata watakiwa kuwa na mbinu bora za usimamizi wa elimu ili kuboresha njia za ufundishaji

Posted on: March 5th, 2019

Maafisa Eimu kata wa Halmashauri ya Arusha, wliaya ya Arumeru, wametakiwa kubuni mbinu za usimamizi wa shule wanazozisimamia ili kuboresha njia za ufundishaji kwa walimu, kwa lengo la kupandisha taaluma katika shule na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wanaohitimu darasa la saba katika halmashauri hiyo.

Wito huo umetolewa na Afisa Elimu Msingi, Halmashauri ya Arusha, mwalimu Hossen Mghewa, wakati akizungumza na Maafisa Elimu hao wa ngazi ya kata, katika kikao kazi cha siku moja,  chenye lengo la kukumbushana utekelezaji wa majukumu ya kazi, pamoja na kubadilishana uzoefu kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kikao kilichofanyika ndani ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri  hiyo.


Mghewa amewasisitiza maafisa Elimu hao, kusiwamamia walimu katika maeneo yao na kuhakikisha shughuli za ufundishaji zinafanyika kwa ufanisi pamoja na kuhakikisha walimu hao, wanatumia maarifa katika kubuni na kutengeneza zana za kufundishia kwa kutumia malighafi zinazopatikana katika mazingira yao, pamoja na kutumia zana hizo wakati wa kufundisha,  mbinu ambazo zitakazorahisisha tendo zima la  ufundishaji kwa wanafunzi.

Mghewa amewataka Maafisa hao, kwenda kukaa na walimu kwenye shule zao, kuweka mikakati thabiti ya kuwafundisha wanafunzi kwa kutumia zana rahisi na kuwajengea uwezo wanafunzi wa madarasa ya mitihani mbinu sahihi za kujibu mitihani,  ili kufuta alama D na F kwenye matokeo ya mitihani yao, huku akisisitiza kuwa jambo hilo linawezekana endapo walimu watajituma na kufanya kazi yao kwa bidii na maarifa.

Aidha amewataka Maafisa hao,  kufanya ukaguzi mara kwa mara shuleni, ili kubaini na kutatua changamoto zinazoikabili walimu na wanafunzi katika shule hizo na kuhakikisha tendo la kufundisha na kujifunza linafanyika kwa ufanisi na kwa kufuata misingi na taratibu zote za ufundishaji, huku akisisitiza kusimamia maadili na nidhamu kwa walimu pamoja na kuthibiti utoro kwa waalimu na wanafunzi.

"Msikae ofisini, zungukeni kwenye shule zenu, ili kukagua ufundishaji wa walimu katika maeneo yenu, kagueni kazi za walimu na wanafunzi, kagueni mahudhurio ya walimu na kuhakikisha ufundishaji unafuata misingi na taratibu, hii itawasaidia kubaini changamoto na kuzitatua kwa wakati" amesisitiza Mghewa.

Hata hivyo, amewataka kuwakutanisha walimu wa masomo na kujadiliana na kupeana uzoefu wa mbinu bora  za ufundishaji, jambo litakalowawezesha kujengeana uwezo kati ya walimu wenyewe na kujenga mazingira rafiki ya ufundishaji, kwa lengo la kukuza ufahamu wa KK tatu za  kusoma, kuandika na kuhesabu kwa wanafunzi ili pasiwepo mwanafunzi anayeshindwa kusoma, kuandika na kuhesabu.

Aidha Mghewa ameagiza kuwepo na daftari malumu kwa kila shule, daftari la kutunza kumbukumbu za utendaji kazi ili kurahisha upatikanaji wa taarifa hizo muhimu, pindi zinapohitajika pamoja na kuhamasisha utendaji kazi kwa waalimu.

"Ninaagiza kuwepo kwa  daftari maalumu kwa kila shule, kwaajili ya kutunza kumbukumbu za utendaji kazi wa walimu, naamini taarifa hizo zitaongeza ari kwa waalimu katika kufanya kazi kwa bidii na kuwabaini wale wote wanaofanya kazi kinyume na maadili" amesema Afisa elimu huyo.

Hata hivyo Maafisa Elimu hao, wameridhishwa kikao kazi hicho na kuthibitisha kuwa, kukutana kwao kumewawezesha kupata maarifa mapya kwa njia ya kujadiliana kwa pamoja changamoto, zinazoikabili sekta ya elimu, pamoja na kubadilishana uzoefu miongoni mwao, huku wakisisitiza kutumia maarifa na maelekezo yaliyotolewa, katika kutekeleza majukumu yao kwa lengo la kupandisha kiwango cha taaluma.

Mwenyekiti wa Maafisa Elimu hao wa kata na Afisa Elimu wa kata ya Oljoro, mwalimu Furahini Godson, amesema kuwa, kikao kazi hicho kimewajenga upya na kuahidi kwenda kutumia maarifa hayo kwenye vituo vya vya kazi huku akiahidi kutekeleza maagizo yote pamoja na kutoa ushirikiano ilikufikia malengo ya halmashauri ya kufuta F na D kwa shule za msingi.

"Binafsi ninashukuru uwepo wa kikao hiki,  licha ya kubadilishana uzoefu, kimkao kimetukumbushana  utekelezaji wa majukumu yetu ya kazi, naahidi kwenda kuyafanyia kazi maagizo yote kwa kushirikiana na walimu katika shule zangu na wadau wengine wa elimu" amesema mwalimu Godson.

Kikao kazi hicho kimewakutanisha maafisa Elimu kutoka kata 27 za halmashauri ya wilaya ya Arusha, wanaosimamia jumla ya shule 141 za msingi za halmashauri hiyo.


Afisa Elimu Msingi, Halmashauri ya Arusha, Mwwlimu Hossein Mghewa akizungumza na Maafisa Elimu ngazi ya Kata, wakati wa kikao kazi cha siku moja, kilichofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.


















Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.