• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MAAFISA USTAWI WA JAMII ARUSHA DC , WATOA MSAADA KWA WATU WENYE UHITAJI

Posted on: April 11th, 2022

Na. Elinipa Lupembe.

Katika kuadhimisha siku ya Ustawi wa Jamii Duniani, wataalamu wa Kitengo cha Ustawi wa Jamii wa halmashauri ya Arusha, wameadhimisha siku hiyo muhimu kwa kutoa msaada kwa watu wenye mahitaji maalum,  kata ya oldonyowas, wilaya ya Arumeru.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya Arusha Neema Mwina, amesema kuwa, katikamkuadhimisha siku hiyo muhimu kwao, wamewiwa kutoa msaada wa chakula na nguo kwa watu wenye ulemavu, watoto waishio katika mazingira hatarishi pamoja na wazee, lengo likiwa ni kutatua changamoto zinazowakabili watu hao, katika nyanja za kiuchum na kijamii.

"Tunatambua changamoto zinazowakabili jamii, hasa makundi maalumu ya wenye uhitaji,  leo tumeamua kuadhimisha siku yetu kwa kutoa kidogo tulichonacho kama ishara ya upendo na kuwathamini wahitaji" amefafanua Neema 

Aidha, afisa Utawi Neema ameutaja  msaada uliotelewa ni kilo 300 za mchele, mifuko 4 ya sabuni ya unga, viroba 7 vya nguo, pamoja na katoni moja ya minara ya sabuni, msaada uliotolewa kwa watu 30, kutoka katika vijiji vinne vya kata ya Oldonyowas. 

Hata hivyo wananchi hao waliopata msaada, wameshukuru halmashauri kwa kuwakumbuka watu wenye uhitaji, na kukikiri kuwa wanakabiliwa na hali ngumu ya kimaisha, huku wakitoa wito kwa serikali kuendelea kuwawezesha watu wa wenye uhitaji hata kwa kuwapa mitaji ya kufanya biashara ndogondogo. 

Napenda kuwashukuru sana kwa huduma hii mliyotuletea, tumefurahi sana kwasababu tuko katika hali ngumu ya kimaisha, tuna watoto wanaotutegemea wengine ni wajane na wengine ni yatima, tuna mzigo mzito sana katika maisha. Alisema Martha Mollel mmoja wa waliopokea msaada huo.

Naye mmoja wa wadau walioshiriki katika kutoa msaada huo Yohana Msomba amesema imekuwa ni desturi yao kuitembelea jamii ya watu wenye uhitaji hususani watoto yatima na wale wanaioshi katika mazingira hatarishi, ili kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili na kuitaka jamii kuonyesha upendo kwao badala ya kuwabagua.

Maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani hufanyika wiki ya mwisho ya Mwezi Machi, kila mwaka, kwa mwaka 2022 maadhimisho hayo, yamebeba ujumbe wa “Umoja na Mshikamano katika Kujenga Ulimwengu Mpya wa Kijamii Twende Pamoja”

ARUSHA DC

KaziIendelee✍








Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.