• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MAAFISA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI ARUSHA DC, WAKUMBUSHWA MAJUKUMU YAO.

Posted on: May 29th, 2023


Maafisa Watendaji wa kata na vijiji halmashauri ya Arusha wametakiwa kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi  kwa weledi kwa kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, halmashauri hiyo, Elizabeth Ngobei wakati wa kikao kazi cha kukumbushana maadili ya utumishi wa umma sambamba na utekelezaji wa majuku ya kazi, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo.

Mkuu huyo wa Idara licha ya kuwapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwahudumia wananchi katika maeneo yao, amewakumbusha kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu hasa kwa kuzingatia Sheri, Kanuni, taratibu na maelekezo maalumu ya Serikali.

"Kila mtu anaomuongozo wa majukumu anayopaswa kutekeleza kila siku, kila mtu anafahamu sheria, kanuni na taratibu za kazi lakini zaidi zingatieni na kutekeleza maagizo yanayoshushwa kwenu, kwa kutoka ofisi ya mkurugenzi, kwa kutambua kuwa mnaowajibu wa kufanyakazi kwa niaba ya mkurugenzi katika maeneo yenu" Amesisitiza Elizabeth.

Uwazi na uwajibikaji ndio nguzo kuu ya Utumishi wenu, ni wajibu kisheria kufanya vikao na mikutano ya kisheria kwa kila robo ya mwaka, inayotoa fursa kwa viongozi na wananchi kujadili taarifa za maendeleo ya kata na vijiji pamoja na kuwasomea taarifa za miradi ya maendeleo na taarifa za mapato na matumizi ya vijiji.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Fedha, CPA David Rubibira amewakumbusha watendaji hao kuongeza kasi ya kukusanya mapato pamoja na kuzingatia matumizi sahihi ya fedha hizo za Umma, yaliyoainishwa kwenye miongozo ya Serikali.Ameongeza kuwa vipo vyanzo vya mapato kwenye maeneo yenu, mkiwa kama wasimamizi wa mapato na matumizi ya fedha hizo, hakikisheni zinakusanywa kwa kutumia mashine za kukusanyia Mapato 'POS' na kuweka benki fedha hizo mara baada ya kukusanya na sio kutumia kabla ya kuziweka benki.

"Mnayo dhamana ya kusimamia Mapato na Matumizi katika maeneo yenu, ni vema kutambua kuwa, ni kinyume cha Sheria kukusanya fedha za Umma bila mashine ya 'POS' pia ni kosa kukaa na fedha hizo zaidi ya saa 24 bila kuziweka benki zaidi ni kinyume cha sheria kutumia fedha hizo kabla ya kuziingiza kwenye mfumo wa benki" Amesisitiza Mweka Hazina huyo.

Hata hivyo Mkuu wa Kitengo cha Ugavi, Hilda Mwangamila naye amewakumbusha suala zima la usimamizi wa fedha za miradi ya maendeleo hususani kwenye kipengele cha manunuzi, kwa kuwataka kuzingatia sheria za utekelezaji wa miradi kupita 'force Akaunti na matumizi ya 'local fundi', miradi ambayo kwa sasa Serikali imeelekezwa kutekelezwa kwenye ngazi za Kata na Vijiji.

"Manunuzi mnayoyafanya ni lazima yapitishwe na wajumbe wa kamati za ujenzi kupitia mzabuni aliyechaguliwa, na kuhifadhi nyaraka zote za manunuzi ikiwemo risiti, kuweni na faili za miradi kwenye ofisi zenu, wasilianeni na ofisi ya manunuzi katika hatua zote, ili kuepuka na kuondokana na hoja za ukaguzi na malamiko ya wananchi". Amefafanua Afisa Manunuzi huyo

Hata hivyo Maafisa Watendaji hao, wameushukuru uongozi wa Halmashauri kwa kikao kazi hicho chenye tija na kuahidi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma ili kufikia malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.


"ARUSHA DC Ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"








 

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.