Na Elinipa Lupembe.
Waheshimiwa Madiwani halmashauri ya Arusha wameridhishwa na jitihada kubwa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kisekta, zilizilizofanyika kipindi cha mwaka wa fedha uliomalizika na kuishia tarehe 31 Juni 2022.
Madiwani hao wametoa pongezi hizo mara baada ya Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya hiyo, kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa mwaka wa fedha 2021/2022, wakati wa mkutano Maalumu wa mwaka wa Baraza Madiwani, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Madiwani hao hawakusita kueleza hisia zao juu ya mafanikio makubwa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika halmashauri na kubainisha kuwa, kwa sasa kuna tofauti kubwa za kimaendeleo katika halmashauri hiyo tofauti na miaka iliyopita na kuipongeza serikali ya awamu ya sita.
"Tunaipongeza serikali yetu ya awamu ya sita, tunampongeza Rais wetu, Mama Samia Suluhu, kwa kutuletea fedha za nje ya bajeti kiasi cha shilingi bilini 3 za kutekeleza miradi mikubwa, miradi ambayo imekamilika kwa wakati na tayari inawahudumia wananchi" Wasema Madiwani hao
Mwenyekiyi wa halmashauri ya Arusha, Mhe.Ojung'u Salekwa, ameweka wazi kuwa halmaahauri imafanyakazi nzuri kwa mwaka uliopita na kuahidi kuongeza kasi ya usimamizi wa shughuli za maendeleo ili kugikia lengo la serikali la kuwahudumia wananchi wa halmashauri hiyo.
Diwani wa kata ya Oldonyosambu Mhe. Raymond Lairumbe amesema kuwa, amekuwepo kwenye baraza hilo tangu mwaka 2015, lakini kuna tofauti kubwa ya kimkakati utekelezaji, ambayo inafanikisha shughuli nyingi kukamilika kwa wakati na viwango huku ukusnayaji wa mapato ya halmashauri.
"Mwaka wa fedha 2021/2022, tumeendela kupata hati safi kwa miaka 6 mfululizo, tumekusanya mapato kwa asilimai 94 ambayo haijawahi kutokea, miradi mingi na mikubwa imetekelezwa na kukamilika, yatupasa tujipongeze madiwani kwa usimamizi, tuwapongeze na watalamu kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya kwa sasa" Amesisitiza Mhe. Lairumbe
Naye Diwani wa kata ya Oljoro, Mhe. Sanare Mepalary, licha ya kupongeza jitihada hizo, ametaka halamshauri kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kufikia asilimia 100 pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato, vitakavyowezesha utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa uwanda mpana zaidi.
Naye Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Mhe. Noah Lembris, licha ya kupongeza juhuudi za watalamu kwa kudpshirikiana na madiwani hao, amewataka kwa pamoja kusimamia miradi yankimkakati iliyoanzishwa na halmashauri hiyo, ikiwemo shule za mchepuo wa kiingereza, mashine ya kufyatulia matofali ili miradi hiyo iwe endelevu na kuipatia halmaahauri mapato, kwa kufanya hivyo fedha hizo zitaweza kupunguza changamoto za kuwahudumia wananchi kisekta.
Akiwasilisha taarifa hiyo ya mwaka mkurugenzi Msumi , amebainisha kuwa halmashauri imefanikiwa kukusanya mapato ya ndani kwa 94.9% na kutekeleza miradi ya maendeleo ya bajeti kwa asilimia 78.6 , na kutekeleza miradi ya nje ya bajeti kwa asilimia 70.8 fedha kutoka serikali kuu kupitia tozo, EP4R na UVIKO 19 huku halmashauri ikipata hati safi ya ukaguzi kwa miaka sita mfululizo.
Aidha amefafanua kuwa halmashauri imefanikwa kufanya vizuri kisekta ya Utawala jumla ya watumishi 638 walipandushwa vyeo, watumishi 545 walilipwa malimbikizo ya mishahara na watumishi 54 waliajiriwa huku sekta ya elimu ikipata ufaulu wa 100% na kushika nafasi ya kwanza kimkoa matokeo ya kidato cha sita.
Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa mwaka, umefanyika kwa mujibu wa sheria na kanuni za serikali za mitaa, ukiwa na agenda za taarifa za maendeleo za mwaka wa fedha 2021/2022, uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti, uundaji wa Kamati za Kudumu za halmashauri pamoja na uchaguzi wa wenyeviti wa kamati hizo za kudumu.
ARUSHA DC TUPO YPTAYARI KUHESABIWA
SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI
JIANDAE KUHESABIWA 23.08.2022
PICHA ZA MATUKIO
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.