• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MADIWANI WAISHAURI OFISI YA DED KUSHIRIKISHA WADAU KUWEZESHA WATENDAJI WA KATA USAFIRI WA PIKIPIKI.

Posted on: February 26th, 2023

Na Elinipa Lupembe

Madiwani halmashauri ya Arusha wameishauri Ofisi ya Mkurugenzi kushirikisha wadau wa maendeleo katika mchakato wa kuwawezesha usafiri wa pikipiki watendaii wa kata kama ilivyo adhma ya Serikali ya kuwezesha mazingira rafiki ya utawala bora kwa watumishi wa Umma ili kurahisisha ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Kata zao.

Madiwani hao wametoa ushauri huo wakati wa mkutano wa baraza la madiwani wa kuwasilisha taatifa za maendeleo ya kata kwa robo ya pili ya mwezi Oktoba – Devemba 2022 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Kaimu mwenyekiti wa kikao hicho Mhe. Baraka Simon ametumia fursa hiyo kuishauri ofisi ya mkurugenzi kuwashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuweza kufanikisha upatikanaji wa pikipiki kwa watendaji kata ili  waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na wepesi zaidi.

“Tunatambua mchango mkubwa wa Serikali katika kuwawezesha Watumishi wetu wa Umma katika kutekeleza majukumu yao ya kuleta maendeleo katika Kata zetu, hivyo nitoe ushauri kwa ofisi ya mkurugenzi iwashirikishe na wadau wa maendeleo waweze kutusaidia katika jambo hili kwa wakati.” Ameshauri Mhe. Mesiaki.

Aidha, ushauri huo umekuja mara baada ya waheshimiwa madiwani kuhoji juu ya mpango wa Serikali wa kuboresha mazingira rafiki ya Utawala bora katika ngazi ya Kata na Vijiji ikiwemo ujenzi wa ofisi za kutolea huduma kwa kata ambazo hazina ofisi kama vile Kata ya Kiutu ambayo haina Ofisi za vijiji pamoja na changamoto ya usafiri kwa watendaji wa Kata.

“Tunaishukuru Serikali kwa kuwapatia usafiri wa pikipiki watendaji wa kata zetu, lakini tunaomba pia iendelee kutoa kipaumbele kwa watendaji wa kata zote ndani ya halmashauri yetu ili watendaji hawa weweze kutekeleza majukumu yao kwa wakati.” Amesisitiza Diwani Kata ya Oloirien Mhe. Erick Semboja.


Akijibu changamoto hiyo, kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha na Mkuu wa Kitengo Sheria Monica Mwailolo, amesema kuwa halmashauri imetenga fungu kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya ununuzi wa pikipiki tano ili kuendelea kupunguza changamoto ya usafiri kwa watendaji wa kata.“Tunatambua kuwa changamoto hii ni kubwa kwa watendaji wetu, hivyo sisi kama halmashauri tutaendelea kutenga bajeti kila mwaka kulingana na uhitaji hadi pale changamoto hii itakapo fikia ukomo na watendaji hawa waweze kutekeleza majukumu yao kwa wepesi Zaidi.” Ameweka wazi Kaimu Mkurugenzi Mwailolo

Itakumbukwa kuwa, hivi karibuni serikali ilitoa pikipiki 197 kwa ajili ya Maafisa Watendaji wa kata nchini, halmashauri ya Arusha ikipata mgao wa pikipiki 8 na kuwa na upungufu wa pikipiki 19 kati ya kata  27 za halmashauri hiyo.










Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.