Na Elinipa Lupembe
Madiwani halmashauri ya Arusha, wamewapongeza watalamu wa halmashauri hiyo kwa utekelezaji wa imara wa shughuli za maendeleo zilizoanyika mwaka wa fedha ulioisha wa 2022/2023 pamoja na kumshukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo kwenye halmashauri hiyo.
Madiwani hao wametoa pongezi hizo, mara baada ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2022/2023 wakati wa mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa mwaka, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikano wa halmashauri hiyo.
Akiwasilisha taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, ameweka wazi kuwa, kwa mwaka wa fedha 2022/2023 halmashauri ilipangiwa bajeti ya kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi bilioni 59.4 na kupokea shilingi bilioni 55.3 sawa na asilimia 93.01 na kutumia shilingi bilioni 54.1.
Amesema kuwa Halmashauri imefanikiwa kukusanya mapato kiasi cha shilingi bilioni 4.8 kutoka bajeti ya shilingi bilioni 4.8 sawa na asilimia 101.24.
Aidha ameeka wazi kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 halmashauri imetekeleza miradi ya maendeleo mara baada ya kuidhinishiwa na Bunge shilingi bilioni 11.8 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, mpaka kufikia Juni 2023, halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi bilioni 11.3 na kutumia bilioni 9.3 sawa na 82%.
Msumi amefafanua kuwa, halmashauri ilipokea shilingi bilioni 1 fedha za nje ya bajeti na kutumia milioni 980 sawa na 89.8 huku kukiwa na bakaa ya shilingi milioni 53 kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Hata hivyo waheshimiwa madiwani hao, kwa umoja wao waliipokea na kuipitisha taaa hiyo kwa kuweka wazi kuwa licha ya changamoto nyingi lakini halmashaui imeweza kusimama kidete na kutekeleza majuku yake kwa asilimia 100, kuanzia ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa fedha za miradi ya maendeleo kwa sekta zote, utoaji wa huduma kwa wananchi, hali ya ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwenye mitihani ya Taifa, usimamizi wa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii pamoja na uibuaji wa miradi yenye lengo la kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Qrusha Mhe. Dkt. Ojung'u Salekwa, licha ya kuishukuru serikali yaawamu ya sita chini ya uongozi makini wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuleta fedha nyingi zilizotekelza miradi ya maendeleo, uongozi wa halmashauri kwa ujumla wake, watalamu kwa sekta zote kwa kuiwezesha halmashauri kufanya vizuri kwa mwaka wa fedha uliopita 2022/2023.
"Kwa mwaka wa fedha uliopita halmashauri imeendelea kuoata hati safi ya ukaguzi, tupokea fedha za miradi ya elimu na afya na kuikamilisha kwa viwango vya ubora, miradi yote iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ilipitishwa na kupata 'Clean Sheet', ongezeko kubwa la ufaulu wa wanafunzi kwa shule za msingi na sekondari kwa kufanya vizuri kwenye mitihani ya Taifa, wananchi walipata chakula cha bei nafuu kutoka serikalini, sambamba na ukusanyaji wa mapato uliovuka malengo, ninatoa pongezi kwa wanaArusha Dc wote" amefafanua Mhe. Mwenyekiti huyo
Diwani wa kata ya Oljoro Mhe. Sanare Mepalary, amesema licha kupongeza utekelezaji wa shughuli za maendeleo, amethibitisha kuvutiwa na hali ya kuimarika kwa ukusanyaji wa mapato hasa kwenye chanzo cha Mchanga Mirongoine hali ambayo imefanikisha kuongeza mapato na kuvuka malengo.
Naye Diwani wa viti Maalum CCM, Mhe. Ester Mollel amesema kuwa amefurahishwa na taarifa ya mwaka iliyowasilishwa ikionyesha hali ya ukusanyaji wa mapato kuvuka malengo na kuwataka watalamu kujipanga kukusanya zaidi kwa mwaka huu, ili kuweza kufikia malengo ya serikali ya kuwahudumia wananchi wote.
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIANE KUIJENGKUIJENGA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.