Na Elinipa Lupembe
Maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari kata ya Moivo mradi ambao uko katika hatua za awali za utekelezaji waje.
Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 584.2 fedha kutoka Serikali Kuu kupitia Program ya Kuboresha Miundombinu ya Elimu kwa Shule za Sekondari (SEQUIP), ikiwa ni utekelezaji wa makati wa serikali wa kuhakikisha kila kata inakuwa na shule ya sekondari.
Mradi huu unajumuisha ujenzi wa jengo la utawala, vyumba 8 Madarasa Maabara 3 za Sayansi, chumba cha Tehama, Maktaba, matundu ya vyoo vya wasichana na wavulana na chumba maalum cha wanafunzi wenye ulemavu, kichomea taka 1, mnara wa tank la maji lenye ujazo wa lita zaidi ya elfu 20
Hata hivyo mradi huo umewezeshwa na wanachi wa kata ya Moivo kwa familia tatu za Marehemu Johnson Lemuruwa, Mosses Lemuruwa na familia Zakayo Sayore Lukumai wa kitongoji cha Ilkirot kwa kutoa eneo lenye ukubwa wa Eka 2 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.
#kaziinaendelea✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.