Maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya watumishi Zahanati ya Likamba kata ya Musa yenye uwezo wa kuishi familia mbili (2 in 1).
Mratibu wa TASAF halmashauri ya Arusha, Grace Makema ameweka wazi kuwa, mradi huo unatekelezwa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na unategemea kugharimu kiasi cha shilingi milioni 70.4.
Kama ilivyo ada ya miradi ya TASAF mradi unatekelezwa na jamii kulingana na taratibu na miongozo ya utoaji wa huduma za jamii kwenye sekta ya afya.
Aidha lengo la mradi huo ni kuboresha huduma utoaji na uoatikanaji wa huduma za afya karibu na wananchi.
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#KaziInaendelea✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.