Maendeleo ya ujenzi wa chumba kimoja cha darasa na matundu matatu ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi wenye Mahitaji shule ya Msingi Ngaramtoni
Mradi huu unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 31.3 fedha kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Fursa sawa katika Ujifunzaji Bora kwa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST).
Ujenzi huo uko katika hatua za kupandisha kuta na unategemea kukamilika mwisho mwa mwezi Juni, 2023.
Ikumbukwe kuwa, miradi hiyo ya ujenzi wa miundombinu shule za msingi ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, Sura ya tatu Ibara ya 79 kifungu (q)Kukarabati miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na kifungu (C)Kuboresha uratibu na usimamiaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.