Na Elinipa Lupembe.
Hivi karibuni Serikali ilitoa fedha kwaajili ya ujenzi wa vituo vya walimu ambavyo vinalenga kuwasaidia walimu kuendelea kupata mafunzo kupitia mifumo mbalimbali kama vile vile mafunzo ya walimu kazini (MEWAKA) ili kuwarahisishia walimu kupata weledi wa kufundisha madarasani.
kituo cha walimu Ilkurot kata ya Lengijave ni mojawapo ya vituo hivyo vipya ambapo ujenzi huo utakapokamilika, serikali inategemea kupata matokeo chanya ya ufaulu wa wanafunzi kutokana na walimu kupata mbinu mbalimbali za ufundishaji kwani walimu kutoka kada zote na sehemu mbalimbali watakutana hapo na kujfunza kwa pamoja.
Hata hivyo, kituo hicho kinagharimu kiasi cha shilingi milioni 22 mpaka kukamilika kwake ikiwa ni pamoja na ununuzi wa samani pamoja na vifaa vya TEHAMA na kufanya halmashauri ya Arusha kuwa na jumla ya vituo vitano katika Kata tano za halmashauri hiyo.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.