Na Elinipa Lupembe
Maendeleo ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na amatundu sita ya vyoo, shule ya msingi Olkejenderet kata ya Lengijave.
Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 81.7 fedha za Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF, miradi hiyo inafadhiliwa na nchi zinazosafirisha mafuta Duniani - OPEC kwa lengo la kuboredha miondombinu ya utoaji wa huduma za jamii kwenye sekta za elimu.
Kukamilika kwa ujenzi wa madarasa haya, unakwenda kuboresha miundombinu ya shule na kuwezasha wanafunzi kujifunza katika mazingira rafiki.
Ikumbukwe kuwa, Serikali kupitia, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ilitoa fedha kiasi cha shilingi milioni 507.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 6 ya maendeleo kwa ngazi ya jamii kwenye sekta ya Elimu na Afya.
Miradi yote itatekelezwa na jamii kwenye maeneo husika kwa muda wa miezi 12 kulingana na taratibu na miongozo ya utekelezaji wa miradi ya TASAF.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.