Maendeleo ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya awali ya mfano shule ya Msingi Engorika kata ya Lemanyata, yanajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 69.1 fedha kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa fursa sawa katika Ujifunzaji bora kwa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST)
Mradi huo utahusisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na samani zake ikiwemo viti na meza 15 maalumu kwa wanafunzi wa madarasa ya awali, viti na meza 2 za walimu, kabati 2 na shubaka 2 za kuhifadhia vifaa, bembea za kuchezea watoto pamoja na matundu sita ya choo huku matundu mawili yakijengwa kwa ajili ya wananfunzi wenye mahitaji maalum.
Ujenzi huo uko katika hatua za kupandisha kuta na unategemea kukamilika mwisho mwa mwezi Juni, 2023.
Ikumbukwe kuwa, miradi hiyo ya ujenzi wa miundombinu shule za msingi ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, Sura ya tatu Ibara ya 79 kifungu (q)Kukarabati miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na kifungu (C)Kuboresha uratibu na usimamiaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.