Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Abdulrahaman Kinana ametoa wito kwa viongozi wa chama hicho kuwa mstari wa mbele katika kukemea vitendo vinavyochangia mmomonyoko wa maadili na kukiuka mila,Tamaduni na Desturi ikiwa ni Pamoja na kusimamia kikamilifu suala la malezi katika jamii ili kuwa na jamii inayoweza kulisaidia Taifa kuwa na maendeleo.
Akizungumza katika kongamano la Maadili na malezi lililoandaliwa na Jumuiya ya wazazi Tanzania Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Abdullahaman Kinana amesema ili Taifa lolote liwe na maendeleo linapaswa kuhakikisha suala la maadili na malezi bora linapewa kipaombele kwani ndiyo msingi wa kuwa na watu wanaoweza kusimamia shughuli za maendeleo na ustawi wa jamii kwa umjula.
Kinana alieleza kuwa Maadili yapatikana kutokana na malezi,na mafunzo huku akitaja wanaofanya kazi hii yakusimamia malezi na maadili kwanza ni familia ambapo alisema familia ndiyo msingi wa uwepo wa jamii ambapo kila mtu anatokea hivyo iwapo familia haita muandaa mtoto kuwa mtu bora pindi anapofikia umri wa utu uzima upo uwezekeno mkubwa wa kuwa na watu wasiowajibika na kulisaidia Taifa,pili jukumu la malezi lipo mikononi mwa jamii kwani inayodhamana ya kusimamiana maadili na tatu ni shule kuanzia awali mpaka vyuo vikuu,
“maadili ni mema ni muunganiko wa tabia zinazotokana na wajibu unaofanywa na kundi la watu katika eneo Fulani ambao wameamua kuishi kwa mfumo unaozingatia misingi ya kuheshimiana,kusaidiana,kushauriana na kukemeana pale wanapobaini kuwepo kwa baadhi yao wanaokwenda kinyume na utaratibu kwa kuzingatia Tamaduni zao”
“wazazi wanapaswa kuhakikisha wanamuandaa mtoto katika misingi imara na bora itakayomsaidia kukabiliana na tabia zianzoweza kubadilisha mwenendo wa Maisha yake lakini pili jamii inaowajibu wa kukemea na kukataa vitendo vyote vinavyopotosha maadili katika maeneo yao”alisema Kinana
Alisema taasisi kama serikali,madhehebu ya dini yanaomchango mkubwa katika kuhakikisha jamii inakuwa na maadili yanayoweza kutoa nafasi ya kukataa vitendo na kauli zinazopingana na utamaduni uliopo ikiwemo kukataa vitendo vya rushwa,Ubaguzi na mengine yanayofanana na hayo
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.