Na Elinipa Lupembe
Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara ya inayojengwa kwa kiwango cha lami, yenye urefu wa Kilomita 18, kutoka Mianzini, Olemringaringa - Ngaramtoni ya Juu na Olemringaringa mpaka Timbolo, halmashauri ya Arusha.
Mhe. Dkt. Mpango ameweka jiwe la msingi na kuzungumza na wananchi katika eneo la Ngaramtoni kata ya Olturumet na kueleza manufaa ya barabara hiyo kwa wananchi kijamii na kiuchumi pia.
Akisoma taarifa ya mradi huo, Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Barabara Tanzania - TANROAD, Mhandis, Rogatus Mativila, amesema kuwa,
Serikali kupitia wakala wa barabra ikiwa ni sehemu ya kuboresha mtandao wa barabara za lami nchini na kupembendezesha miji yetu, imetoa shilingi bilioni 22.2 kwa ajili ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa Km 18.
Amesema kuwa barabara hiyo ya Km 18 inajumuisha mtandao huo wa barabara ya kuanzia Mianzini - Olemringringa mpaka Forest Km 12.4, Olemringaringa - Timbolo Km 2.9.5, kipande cha Ngaramtoni- Selian Hospitali Km 2.15, Seliani mpaka Ngaramtoni Sokoini Mita 500 pamoja na Ngaramtoni Sokoni - kuunganisha barabara ya Arusha Namanga Km 0.18.
Ameongeza kuwa, mradi unahusisha ujenzi wa daraja moja kubwa kwenye mita 13 mto Lekasenge, makaravati makubwa 8, madogo 45 , taa za barabara kwenye maeneo ya makazi ya watu.
"Usanifu wa barabara hii umezingatia ubora na mahitaji ya jamii, ikiwa na upana wa Mita 9. 5 na Mita 1.5 sehemu ya watembea kwa miguu katika maeneo ya mjini na katika maeneo ya vijijini yatakuwa na mabega hadi kufikia Mita 2.5 kwa watembea kwa miguu". Ameweka wa Mhandisi Mtwivila.
Ameongeza kuwa, mradi huu unatekelezwa wa asilimia 24 na kampuni kutoka nchini China kwa shilingi Bilioni 22.2 bila VAT na mkataba ulioanza Januari 2022 utakamilika mwaka 2023 huku
Mhandisi Mshauri akiwa ni TANROAD Arusha.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
KaziInaendelea
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.