• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MALAIGWANANI WAAZIMIA KUKOMESHA TOHARA NA NDOA ZA UTOTONI

Posted on: August 23rd, 2020

Na Elinipa Lupembe.

   Viongozi wa mila wa kabila la kimaasai nchini Tanzania, wamekubaliana kuungana na serikali na asas zisizo za serikali, kupinga ukatili wa kijinsi kwa wasichana, ukatili uliofanya na kabila hilo kulingana na mila na desturi za kabila hilo.

    Viongozi hao wa kimila, maarufu kama Malaigwanani, wamekiri kukomesha tabia za tohara kwa watoto wa kike pamoja na kuozesha watoto katika umri mdogo,na kukubaliana kuwaacha watoto hao wasome kama ilivyo malengo ya serikali na haki za mtoto pia.

   Hayo yamethibitishwa na Katibu wa mila za kimaasai Tanzani, Mzee Amani Lukumai, alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye Bonanza la Mtoto wa Kike, liliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Bangata halmáshauri ya Arusha.

        Katibu huyo wa mila, aliyevuta hisia za watu wengi, ameweka wazi kuwa katika kikao, cha Malaigwanani, kilichofanyika siku za hivi karibuni, wamekubaliana kuachana na mila hizo potofu, mila zinazomkandamiza mtoto wa kike, badala yake wameahidi kumsimamia mtoto wa kike, aweze kupata haki zake za msingi ikiwa ni pamoja na elimu.

       "Sisi viongozi wa mila ya kimaasai nchini, tumepitisha azimio la kuungana na serikali yetu, kumtetea mtoto wa kike kutokana na ukatili dhidi yake, kwa kuhakikisha tohara zinakomeshwa, hakuna ndoa za utotoni, hakuna kumchagulia mtoto mchumba, badala yake tutamsimamia mtoto wa kike asome" amesema katibu wa mila, mzee Lukumai.

    Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, wakati wa kufunga Bonanza hilo, Afisa Maendeleo ya Jamii, halmashauri hiyo, Angela Mvaa, amewasisitiza, watoto wa kike kutumia fursa walioyonayo ya kuwa shuleni, kuzingatia masomo, kwa kuwa wazee na wazazi wao wamekubali kuachana na mila na desturi zao, na kuwaacha wasome.

    "Ni wasihii wasichana, wazazi wenu wamekubali kuachana na mila za tohara na ndoa za utotoni, wamekubali kuwatetea na kuwaacha msome, tumieni fursa hiyo, kusoma kwa bidii ili muweze kutimiza ndoto zenu, fursa ambayo wasichana wengi wa kabila la kimaasi waliikosa, tambueni mna bahati elekezeni juhudi zenu kwenye masomo" amesisitiza Angela

      Namnyaki Salekwa mwanafunzi wa shule ya msingi Ilkiding'a, amewashukuru viongozi hao wa mila, kwa kukubali kuwatetea watoto wa kike, kwa kuwa mila hizo zilizuia wasichana wengi, kuendelea na masomo, na hata wengine kushawishiwa kufanya mitihani vibaya ili wafeli waolewe, na wengine kubeneshwa mimba na kutoroshwa, wangali wanafunzi.

  "Tumefurahi kusikia wazee wetu, wameamua kuachana na mila hizo potofu za kumkandamiza mtoto wa kike, mila zilizowaumiza na kuharibu ndoto za mtoto wa kike, kwa vile wameamua sasa tusome, hatuta waangusha, tutasoma kwa bidi ili tuwathibitishie wazee wetu maamuzi waliyoyafanya sahihi kwa mtoto wa kike"amesema Namnyaki

     Naye Mkurugenzi wa shirika la Center for Women and Children Development (CWCD),  Hindu Mwego, amesema kuwa, baada ya mapambano ya muda mrefu dhidi ya ukatili  kwa mtoto wa kike, hatimaye jamii imeanza kuelewa, huku  hali ya ukatili kwa mtoto wa kike ikianza kupungua, licha ya changamoto nyingi lakini  wanaamini kwa kushirikiana na viongozi wa mila kuendeleza mapambano iko siku, mila hizo potofu zitatokomea kabisa.

   Hindu ameongeza kuwa, uwepo wa Bonanza hilo liliowakutanisha watoto,  licha ya kuwapatia watoto burudani na jumbe zenye mafunzo, limeambatana  na maonesho ya shughuli za mikono wanazozifanya watoto shuleni wakiwa kwenye klabu zao za kupinga ukatili dhidi ya Mtoto wa kike, klabu ambazo zinasimamiwa na walimu kwa udhamini wa shirika la CWCD la mjini Arusha.

      Bonanza hilo la mtoto wa Kike, limeandaliwa na halmashauri kwa kushirikiana na shirika la CWCD, kwa ufadhili wa shirika la Foundation for Civil Society na kuwakutanisha wanafunzi wa shule 14 za msingi na sekondari za halmashauri ya Arusha, likiwa na lengo la kumjengea uwezo mtoto wa kike kujiamini, kujithamini ili kuweza kulinda na kutetea haki zake dhidi ya ukatili wa mtoto wa kike.


PICHA ZA MATUKIO YA BONANZA



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.