• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MAMA SAMIA AWANUSURU WATOTO YATIMA KWA NJAA ARUSHA DC.

Posted on: July 20th, 2022

Na Elinipa Lupembe

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mama Samia Suluhu Hassan, amewanusuru kwa njaa watoto yatima, halmashauri ya Arusha kwa kutoa Kilo 500 za mchele kwenye vituo 10 vya kulelea watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.

Wakizungumza wakati wakikabidhiwa chakuka hicho na Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Arusha, kwa niaba ya mheshimiwa Rais, walezi wa vituo hivyo wamekiri kuwepo kwa uhaba wa vyakula kwenye makazi ya kulelea watoto yatima kwa sasa, zoezi lililofanyika kwenye ofisi za makao makuu ya halmashauri hiyo.

"Tuseme tu wazi, kwa kutupa chakula hiki, mheshimiwa Rais amewanusuru watoto yatima kwa njaa, kutokana na ukweli kwamba, kwa sasa vituo vyetu vinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyakula na mahitaji mengine ya kila siku". Wamesistiza viongozi  wa vituo hivyo.

Licha ya kumshukuru mheshimiwa Rais na serikali ya awamu ya sita, kwa msaada huo wa chakula, walezi wa vituo hivyo, wamesistiza kuwa chakula hicho kimekuja wakati muafaka kutokana na kuwepo kwa tatizo la upungufu wa vyakula katika makazi mengi ya kulea watoto yatima kwa sasa.

Mkurugenzi wa Kituo cha Huruma Ophanage kilichopo kijiji cha Kiserian kata ya Mlangarini, Yohana Msomba, amebainisha kuwa, kwa sasa vituo vya watoto yatima vinakabiliwa na uhaba wa vyakula na mahitaji mengine ya kila siku, hali inayotokana na vituo vingi kutegemea wafadhi kutoka nje ya nchi, wafadhili ambao wamesitisha kuleta misaada, kutokana na athari za UVIKO 19, Vita vya Ukraini pamoja na ukame.

Naye Afisa Ustawi wa Jamii, kituo cha Shalom Center, Glory Swai ameipongeza serikali kwa kutoa elimu bila malipo jambo ambalo limepunguza gharama kwa vituo vya watoto yatima sambamba na kuwawapa fursa watoto yatima kusoma vizuri kama watoto wengine na kutimiza ndoto zao.

"Nikiri wazi kuwa, msaada huu ni wa thamani na alama kubwa sana kwa watoto, inaonesha jinsi ambavyo serikali inawajali watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, tunaishukuru serikali kwa kuwapenda na kuwajali watoto wenye uhitaji" Amesisitiza Dr.Alex Lengeju Mkurugenzi wa Kituo cha Kanani Ophanage Kilichopo Kisongo.

Naye mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amesema kuwa serikali inathamni sana mchango mkubwa unafanywa na Asas za kiraia kwa kutekeleza malengo ya serikali katika sekta ya Ustawi wa jamii husani kwenye malezi ya watoto yatima, hili lilikuwa ni jukumu la serikali, kwa kuthamini kazi hiyo, mheshimiwa Rais ameona ni vyema kutoa chakula ili kuwahudumia watoto hao.

"Mheshimiwa Rais ametoa kilo 500 za mchele kwa vituo 10 vyenye jumla ya watoto 255 wanaoishi kwenye vituo hivyo, niseme tu kwaba mheshimwa Rais anawajali na kuwathamini watoto yatima, anatamani watoto hao watimize ndoto zao kama ilivyo kwa watoto wengine wenye wazazi". Amesistiza Mkurugenzi Msumi.

Hata hivyo Afisa Utawi wa Jamii Kiongozi halmashauri ya Arusha, Beatrice Tengi, amethibitisha kuwa, kutokana na ufuatiliaji unaofanywa na ofisi yake umebaini, makazi ya Watoto yatima kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa chakula na mahitaji mengine, kwa kuwa baadhi ya wafadhili waliokuwa wakitegemewa kutoa misaada kusitisha huduma hiyo, jambo lililosababishwa na athari za UVIKO 19 pamoja na vita vya Ukraini.

Ameitaka jamii kushirikiana na serikali kujitoa kuwalea watoto wanaoishi kwenye makao, kwa kutoa msaada wa kitu chochote walicho nacho, ili kuvinusuru vituo hivyo, sambamba na kuisisitiza jamii kuona umuhimu wa kuwalea watoto yatima katika familia zao.

Ikumbukwe kuwa hii ni awamu ya pili ndani ya mwezi mmoja kwa Mheshimiwa Rais kutoa masaada wa vyakula kwa watoto yatima katika halmashauri ya Arusha.

ARUSHA DC

#KaziInaendelea

JIANDAE KUHESABIWA

Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, akimkabidhi mfuko wa kilo 50 za mchele Afisa Ustawi wa Jamii, kituo cha Shalom Center, Glory Swai 

Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, akimkabidhi mfuko wa kilo 50 za mchele   Mkurugenzi wa Kituo cha Huruma Ophanage kilichopo kijiji cha Kiserian kata ya Mlangarini, Yohana Msomba  


Picha ya pamoja ya viongozi wa Halmashauri ya Arusha na wasimamizi wa vituo vya kulelea watoto yatima wakati wa makabidhiano ya chakula kutoka kwa Mhe. Rais mama Samia Suluhu Hassan kwaajili ya kuwanusuru watoto hao dhidi ya njaa


Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi pamoja na Afisa Ustawi wa Jamii kiongozi Halmashauri ya Arusha, Beatrice Tengi wakisaidiana kusogeza mfuko wa kilo 50 za mchele



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.