Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu akipokea Mwenge wa Uhuru 2024 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Qeen Sendiga kwenye viwanja vya shule ya Msingi Migungani, Kijiji cha Migungani, Kata ya Mbuguni wilaya ya Arumeru leo Julai 19, 2024.
Akitoa taarifa ya Mkoa wa Arusha Mhe. Babu amesema, katika mkoa wa Arusha Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa Kilomita 1,189.35 kwenye Wilaya sita na Halmashauri zake saba kwa Mwenge huo kupita Miradi 65 ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 61.6.
Mhe.Babu ameongeza kwa kusema kuwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava ataweka Mawe ya Msingi miradi 18 ya Maendeleo, atafungua mradi 1, atazindua miradi 12 na kutembelea miradi 34 ambayo ipo ni ipo katika sekta za Elimu, Afya, Maji, Miundombinu ya Barabara, Uwezeshaji vijana Kiuchumi, Biashara na Ujasiriamali, Lishe, Klabu za Vijana wapinga Rushwa, Makundi Maalum, Uhifadhi wa Mazingira.
Aidha Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2024 utatembelea Miradi ya Maendeleo iliyowekewa mawe ya msingi na kuzinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ikiwa ni kujionea uendelevu wa miradi hiyo pamoja na kuona unufaikaji wa jamii kutokana na uwepo wa miradi hiyo iliyotekelezwa na Serikali.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 ni "Tunza Mazingira, Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu", ukiwa na Jumbe za Kudumu za Mwenge wa Uhuru za Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malari, matumizi ya Dawa za Kulevya, VVU - UKIMWI na Rushwa sambamba na kuhamasisha wananchi kuzingatia Lishe Bora pamoja na kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kujiandikisha kwenye daftari la Wapiga kura.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.