MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA ARUSHA WILAYA YA ARUMERU.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango anategemea kupokea Mwenge wa Uhuru katika halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru kesho tarehe 23.06.2022, kwenye viwanja vya shule ya sekondari Oldadai ukitoke halmashauri ya Jiji la Arusha.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022, ndugu Sahil Nyanzabara Geraruma atakimbiza Mwenge wa Uhuru Kilomita 90.4, na kupitia jumla ya Miradi 9 yenye thamani ya shilingi Bilioni 4.2 kwenye sekta ya elimu, afya, maji, miundombinu ya barabara na uwekezaji.
Ukiwa katika halmashauri ya Arusha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, atatembeeka na kukagua mradi wa ukamilishaji ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa, shule ya sekondari Oldadai uliogharimu shilingi milioni 40.5, ikiwa milioni 19.4 ni michango ya wananchi na milioni 8.5 ni michango ya Mwenge wa Uhuru na milioni 12.5 fedha ya Serikali Kuu kupitia Tozo za mihamala ya simu. Pia Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru atazindua ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa shule ya sekondari Oldadai, Mradi uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 40 Fedha za mapambano dhidi ya UVIKO-19.
Aidha Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru atatembelea miradi ujenzi wa mradi wa maji wa vijiji 5 Losikito - Mwandeti utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.5, Mradi wa Uwekezaji kiwanda cha Maziwa SIVAT wenye thamani ya shilingi milioni 506, Nyumba maalum ya Warahibu wa Madawa ya kulevya kata ya Olturumet.
Kituo cha kutoa virutubisho kwa watoto wenye utapiamlo Mateves, mradi wenye thamani ya shilingi milioni 2.6 pamoja na Kikundi cha Vijana (WINNER STUNNA) kilichopewa mkopo wa asilimi 4 ya vijana kiasi cha shilingi milioni 10, fedha za Mapato ya ndani ya Halmashauri.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru atazindua Kiwanda cha maziwa SIVAT, mradi wenye thamani ya shilingi milioni 506 ikiwa ni fedha za michango ya wananchi na mradi wa barabara ya Martenity Africa wenye thamani ya shilingi milioni 897 fedha kutoka Serikali Kuu.
Kadhalika Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ataweka jiwe la Msingi kwenye kituo cha Afya Oloirieni, Mradi uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 450 huku shilingi milioni 400 zikiwa ni fedha za Mapato ya Ndani kupitia fidia ya deni la Lakilaki na shilingi milioni 50 fedha kutoka Serikali Kuu.
Licha ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, atazindua Muunganiko wa Klabu ya Wapinga Rusha na Skaut (TAKUSCA) katika shule ya sekondari ya Oldadai pamoja na kutatoa Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru kwa wananchi wa halmashauri ya Arusha.
Hatimaye Mwenge wa Uhuru utakesha kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Halmashauri ya Arusha, eneo la Sekei kata ya Kiutu, na kisha kukabiidhiwa kwenye halmashauri ya Wilaya ya Meru.Mkuu wa Wilaya anawakaribisha wananchi wote kushiriki kwenye mapkezi ya Mwenge wa Uhuru, kwenye miradi pamoja na mkesha.
MWENGE WA UHURU Hoyeeeeeeee
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.