• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MBUNGE NOAH LEMBRIS:  ARUMERU MAGHARIBI IMEPATA FEDHA NYINGI ZA MIRADI YA MAENDELEO KWA AWAMU YA SITA.......

Posted on: December 20th, 2022

Na Elinipa Lupembe


Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Mhe. Noah Lembris amesema kuwa katika kipindi cha awamu ya sita, Jimbo lake limepata fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo tofauti na awamu zilizotangulia.


Mhe. Noah ameyasema hayo wakati akitoa salamu kwa wananchi waliohudhuria hafla fupi ya makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa vyumba 38 vya madarasa halmashauri ya Arusha, hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mringa.


Mbunge huyo ameeleza mafanikio ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo Jimbo hilo la Arumeru Magharibi limepata fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za Elimu, Afya, maji na miundombinu ya barabara, miradi ambayo imeondoa kero zilizokuwa zikiwakabili wananchi wa jimbo hilo kwa muda mrefu.


Amesema kuwa licha ya kuwa mwaka 2022 serikali imetoa shilingi Milioni 760 za kujenga madarasa 38 kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023, amebainisha kuwa fedha hizo ni sehemu ndogo ya fedha ambazo serikali ya awamu ya sita imezitoa jimboni humo.


"Milioni 760 ni sehemu tuu ya miradi iliyotekelezwa na Serikali ya CCM ndani ya ndani ya Jimbo hili, lakini serikali imetoa shilingi  Bilioni 22 za ujenzi wa barabara yenye urefu wa Km 18 ya kutoka Mianzini, Timbolo, Sambasha mpaka Ngaramtoni, yote hayo ni mafanikio makubwa ndani ya Jimbo letu la Arumeru Magharibi kwa muda mfupi sana". Ameweka wazi Mhe. Noah.


Ameongeza kuwa wananchi wa Arumeru Magharibi wana kila sababu ya kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa miradi mingi ya maendeleo ambayo inatatua kero na changamoto nyingi katika hizo sambamba na kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi.


Aidha hakusita kuwawapongeza watendaji  wote kuanzia ngazi ya wilaya, halmashauri na kata na shule kwa kuhakikisha miradi  yote inatekelezwa kwa ubora kwa kuzingatia viwango vinavyoendana na thamani ya fedha zilizotolewa na serikali 'value for money'.


ARUSHA DC

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.