Na Elinipa Lupembe
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa amewaongoza wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kata ya Mlangarini kupanda miti ikiwa ni ishara ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo 27, Januari, 2023.
Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika mapema asubuhi ya leo kwenye eneo la shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza ya Enyorata inayomilikiwa na halmashauri ya Arusha.
Mwenyekiti Ojungu amebainisha kuwa zoezi hilo la kuotesha miti ni muhimu kwa wanaarusha DC, na zaidi ni ishara ya upendo kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesisitiza kuwa uwepo wa miti shuleni hapo utasiadia utunzaji wa mazingira hayo makame pamoja na upatikanaji wa hewa safi katika eneo hilo.
"Kuotesha miti ni jambo la moja lakini, kwa kumbukumbu ya siku hii muhimu ya Mheshimiwa Rais, miti hii inatakiwa kutunzwa vizuri zaidi kwa umuhimu wake ikiwa ni kumbukizi ya mama yetu" . Amesema Mwenyekiti Ojung'u
Nao wanafunzi wa shule ya Msingi Enyorata wameshiriki zoezi la kuoetesha miti na kuahidi kuitunza miti hiyo kwa ajili ya afya ya mama Samia na kwa afya zao.
Nathan Piniel mwanafunzi wa darasa la IV, wamemtakia kila la kheri mama Samia na kuweka wazi kuwa wanampenda sana, na wanaamini ni mama wa Watanzania wote.
"We all love mama Samia, is the mother of our country, we plant the threes to show a real love to her" Said Herieth Marick
Awali jumla ya miti 1,200 inatarajiwa kueoteshwa leo kwenye shule 11 za msingi na Sekondari za kata ya Mlangarini ikiwa ni maalum kwa kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"ARUSHA DC Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#KaziInaendelea✍✍✍
PICHA ZA MATUKIO YA UPANDAJI MITI
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.