Na. Elinipa Lupembe.
Katika kipindi cha Miaka 4 ya Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, kupitia miradi ya Lipa kutokana na matokeo 'Education Payment for Result' (EP4R), imeweza kuboresha miundombinu ya shule za kata nchini.
Shule ya sekondari Mlangarini, halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, ni miongoni mwa shule zilizonufaika na miradi hiyo kwa kuipandishwa hadhi na kuwa shule ya kidato cha tano na cha sita 'High School', na kuleta mamilioni ya fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo ya kata, ili iweze kuendana na hadhi ya shule nyingine za kidato cha tano na sita.
Mwaka wa fedha 2016/2017, Serikali ilianza kutoa fedha, kiasi cha shilingi milioni 250, fedha zilizofanikisha ujenzi wa Bweni la wasichana 80, ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa, ukarabati wa maabara tatu za masomo Sayansi pamoja na ujenzi wa vyoo vya wanafunzi.
Hata hivyo kutokana matokeo mazuri ya usimamizi wa miradi hiyo, mwaka huu wa fedha 2018/2019, serikali ilitoa fedha nyingine shuleni hapo, kiasi cha shilingi milioni 110, kwa ajili ya ujenzi wa Maktaba na ukarabati wa bwalo la chakula, ujenzi ambao kukamilika kwake umeleta mapinduzi makubwa ya kielimu kwa wanafunzi na walimu wa shule hiyo.
Mkakati huo wa serikali ya awamu ya tano, wenye lengo la kupandisha kiwango cha taaluma shuleni, kwa kuwezesha mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia, umeendelea kuleta mafanikio chanya kwa shule za msingi na sekondari nchini.
Aidha, uongozi wa halmashauri ya Arusha, unawataka wananchi na wadau wote wa elimu ndani na nje ya halmashauri, kuunga mkono juhudi za Dkt. John Magufuli na Serikali yake ya awamu ya tano, kwa kuchangia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya shule za serikali, ili kuhakikisha mtoto wa kitanzania kutoka familia masikini naye anapata elimu katika mazingira bora na rafiki.
#TULIAHIDI#TUMETEKELEZA#HAPA#KAZI#TUU#
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.