• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MIAKA 61 YA UHURU WATANZANIA WATHIBITISHA MAFANIKIO MAKUBWA SEKTA YA ELIMU UCHUMI NA AFYA...

Posted on: December 8th, 2022

Na Elinipa Lupembe - ARUSHA DC

Kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika, wananchi halmashauri ya Arusha wilaya ya Arumeru wamekiri kuwepo mafanikio makubwa nchinim katika sekta za elimu, uchumi na afya, yaliyotokana na juhudi za serikali za mapambano dhidi ya maadui ujinga, umaskini na maradhi.

Wananchi hao wamedhibitisha hayo, wakati wa Mdahalo maalum uliowashirikisha wakazi wa halmashauri ya Arusha, uliobeba mada ya "Miaka 61 ya Uhuru na Mapambano dhidi ya maadui Ujinga, Umaskini na Maradhi".

Mdahalo huo uliongozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Mwl. James Mchembe, wananchi wamebainisha matokeo ya mapambano dhidi ya ujinga yanayojidhihirisha wazi, kutokana na ongezeko la wasomi lililotokana na uwepo wa shule na vyuo vya kati na vikuu katika mikoa yote nchini, uliotoa fursa ya kila mtanzania kupata elimu.

"Kwa sasa Serikali imetoa fursa kila mtanzania kuwa na haki ya kupata elimu, kuanzia elimu ya awali mpaka chuo kikuu, tofauti kabla ya Uhuru elimu ilitolewa kwa ubaguzi, kubwa zaidi uwepo wa shule za serikali kila kata, za mashirika  na  binafsi kwa ujumla zimepanua wigo wa wananchi kuondokana na ujinga" Mwl. Emanuel Mkonongo.

Ameongeza kuwa baada ya Uhuru serikali ilijikita kwa wananchi wake kufuata ujinga kwa kuhakikisha wananchi wanajifunza Kusoma, Kuandika na kuhesabu, kwa sasa Taifa linatafuta wasomi wataalam wa fani mbalimbali na si wasomo wa KKK tatu.

Bw. James Magumba amezungumzia hali halisi ya mabadiliko katika sekta ya usafiri na usafirishaji, watanzania wakiwa wanajivunia maendeleo ya miundombinu ya barabara zinazofikika katika mikoa  yote Tanzania hadi katika maeneo ya vijijini.

"Kwa sasa watanzania tunasafiri kutoka eneo moja kwenda jingine kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi, bila ya kuwa na kikwazo, tofauti kubwa baada ya Uhuru mtu alisafiri zaidi ya siku 4 sehemu ya kufika kwa siku moja,  Mungu ibariki Tanzania" Amebainisha Bw. Magumba

Victo Karia amezungumzia mabadiliko katika sekta ya afya kuanzia mtu binafsi, upatikanaji wa huduma za afya, uwezeshwaji wa upatatikanaji wa huduma za afya pamoja na ushirikishwaji wa jamii katika kupambana na magonjwa kupitia watoa huduma ngazi ya jamii.

Bw. Karia amebainisha mabadiliko ya kiafya yaliyotokana na mapambano dhidi ya ujinga na umaskini yaliyomuwezesha mtanzania mwenyewe kufahamu namna ya kujikinga na maradhi kupitia lishe bora na usafi wa mtu na mazingira, jambo ambalo zamani watu wengi walipoteza maisha kutokana na  magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, surua, utapiamlo magonjwa ambayo watanzania wa sasa wamefahamu namna ya kujikinga.

Serikali imefanikiwa kuboresha sekta ya afya kwa kusogeza huduma za afya, karibu na wananchi kwa kuhakikusha kila kijiji kina zahanati, kata ina kituo cha afya, hosptali ya wilaya na kuwa hosptali za rufaa za mkoa, jambo ambalo licha ya kurahisisha upatikanaji wa matibabu, limeondoa msongamano hospitalini.

Mdahalo ni maalum kuelekea maadhimisho ya sikuu ya Uhuru wa Tanganyika tarehe 09.12.2022.uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano shule ya Msingi Green Acres kata ya Kikata


yARUSHA DC

KaziIendelee✍✍


PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA MDAHALO




Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.