• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Miche ya miti, utalamu wa uoteshaji ni bure Arusha DC

Posted on: March 28th, 2018

Halmashauri ya Arusha imezindua siku ya upandaji miti kitaifa, huku ikiwa imejipanga kutoa miche ya miti bure  kwa wananchi na taasisi ndani ya halmashauri hiyo.

Akizungumza wakati wa zoezi la upandaji miti lililofanyika kiwilaya katika kijiji cha Ilkiding'a, mgeni rasmi Afisa Utumishi halmashauri ya Arusha, Selemani Sekiete amesema kuwa, halmashauri imeandaa mkakati thabiti wa kupanda miti kwenye maeneo yote, kwa kutoa miche ya miti kwa taasisi na watu binafsi bila kulipia, kutoka kwenye kitalu cha miti cha halmashauri.

Sekiete ameongeza kuwa licha ya kutoa miche hiyo bure pia watalamu watatoa ushauri na mafunzo juu ya uoteshaji na utunzaji wa miti hiyo, sambamba na ushauri wa uoteshaji miti inayoendana na mazingira halisi ya eneo la muhitaji.

"Mwananchi anayehitaji miche ya miti, afike kwenye ofisi za halmashauri,atapatiwa miche bure pamoja na ushauri wa kitaalamu kutoka kwa watalamu wetu namna ya kutunza miti hiyo" amesema Sekiete.

Aidha amefafanua kuwa kwa sasa, wananchi wanapaswa kupanda miti kama zao la biashara, zao linaloruhusu na ufugaji wa nyuki katika miti hiyo na kuwataka vijana kujikita katika upandaji wa miti katika maeneo yao.

Josephat Likindambeki mwananchi aliyeshiriki zoezi la upandaji miti, amethibitisha kupatiwa miche bure na kusema kuwa jambo hilo linawahamasisha wananchi kupanda miti na kufahamu umuhimu wa kupenda kutunza mazingira yao.

"Zamani sikufahamu umuhimu wa kupanda miti wala kutunza mazingira, nilipokwenda halmashauri kuomba miche wakanishauri na kunielekeza aina ya miti ya kuotesha na umuhimu wake kwa mazingira" amesema Likindambaki.

Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Afisa Wanyamapori halmashauri ya Arusha, Tabea Mollel amesema kuwa kitengo cha Maliasili kimepanga kupanda miti zaidi ya milioni 2.5 kwa mwaka huu pamoja na uhamasishaji wa ufugaji wa nyuki katika miti hiyo ili kupata malighafi za viwanda zitakazotokana mazao ya miti na nyuki.

Hata hivyo Mollel amesema kuwa licha ya jitihada za kupanda miti kwa wingi bado miti hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukame kwa baadhi ya maeneo na mifugo kwa maeneo ya wafugaji, changamoto inayopoteza zaidi ya aslimia 30% ya miti inayopandwa kila mwaka.

Ameongeza kuwa, licha ya changamoto hizo bado wanaendelea kutoa elimu kwa wafugaji kufanya ufugaji wa kisasa wenye tija wa kutumia eneo dogo ili kutunza mazingira yao na kuwa na mifugo michache na bora.

Awali watumishi wa halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na wananchi na wakazi wa kata ya Ilkiding'a, wamepanda jumla ya miti elfu 6, kwenye chanzo cha maji cha Saiteru katika kijiji cha Ilkiding'a katika kuazimisha siku ya upandaji miti kitaifa, yenye kauli mbiu ya 'Tanzania ya kijani inawezekana, tupande miti kwa maendeleonya viwanda'.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.