Halmashauri ya Arusha imepokea fedha kiasi cha shilingi milioni 100 kutoka serikali kuu kupitia mradi wa kuboeresha miundombinu ya shule za sekondari - SEQUIP kwa ajili ya kukarabati wa mabweni manne ya zamani shule ya sekondari Mringa.
Ukarabati wa mabweni hayo ya wasichana, utawezesha kulaza jumla ya wanafunzi 160 huku kila bweni ikiwa na uwezo wa kulaza wanafunzi 40.
Shule ya sekondri Mringa ni miongoni mwa shule kongwe zinazofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa yenye kidato cha I ampaka cha VI, ikuwa na jumla ya wanafunzi 1,962 wavulana 617 na wasichana 1,345 huku wanafunzi 375 ni wa kidato cha tano na cha sita.
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.