• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MILIONI 130 ZA MAPATO YA NDANI ZAEPUSHA VIFO VYA MAMA NA MTOTO HOSPITALI YA OLTURUMET - ARUSHA DC

Posted on: August 27th, 2020

Na. Elinipa Lupembe.

   Kufuatia mkakati wa serikali ya awamu ya tano, wa kupunguza na kuondoa kabisa vifo vya mama na mtoto  wakati wa kujifungua nchini, halmashauri ya  Arusha imefanikisha ujenzi wa jengo la mama na mtoto, kwenye hospitali yake ya wilaya ya  Olturumet na tayari limeanza kutumika.

    Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, alipotembelea hospitalini hapo, kujionea hali ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi, amesema kuwa, jengo hilo limesaidia kutoa huduma kwa kinamama wajawazito wa maeneo hayo, na kupunguza vifo vya mama na mtoto pamoja na kupunguza wimbi la wajawazito kujifungulia nyumbani.

  Ameongeza kuwa, kukamilika kwa jengo hilo ambalo tayari limeweanza kutoa huduma kwa kina mama wajawazito, mradi ambao umetokana na kodi za wananchi wa halmashauri hiyo, kodi ambazo wananchi hulipa kwa halmashauri hiyo na asilimia 40 ya mapato hayo, hutumika kwenye miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo za halmashauri hiyo.

    "Halmashauri imetumia shilingi milioni 130, fedha za mapato yake ya ndani, tunaendelea kujivunia uwezo wa watanzania kuanza kujitegemea kwa maendeleo yetu na kuacha kutegemea wageni, jengo zima limejengwa kwa fedha za kodi za wananchi, zinazolipwa na wananchi wa halmashauri ya Arusha, tuendee kujivunia vyetu"amesisitiza mkurugenzi huyo.

   Hata hivyo, wakinamama waliofika hospitalini hapo kwa ajili ya kujifungua, wameishukuru serikali ya awamu ya tano, imafanya mabadiliko makubwa kwa kuboresha huduma za afya hadi maeneo ya vijijini, jambo lililosababisha wao kuacha kujifungulia nyumbani na kufika hospitali ambapo kuna huduma bora.

    Eva mollel (36), amethibitisha kuwa zamani walijifungulia nyumbani kwa kuwa, hosptali kulikuwa na usumbufu sana, hakukuwa na dawa, hakuna vitanda, wajawazito walilazwa wawili wawili kitanda kimoja au pengine chini, lakini kwa sasa hali imebadilika sana, kina mama wanavutiwa kuja hosptali kwa kuwa wanapata huduma bora.

   Mganga mfawidhi Wodi ya Wazazi hospitali ya Olturumet Dkt. Festus Kinabo, amesema kuwa, uwepo wa jengo hilo hospitalini hapo, umeongeza idadi ya wajawazito kujifungulia hospitali tofauti na awali, jambo ambalo limesababisha kuzalisha wastani wa watoto 5 kwa siku na watoto 150 huku vifo vya mama na mtoto vikipungua kwa zaidi ya asilimia 97.

   Aidha Dkt. Kinabo ameweka wazi kuwa, licha ya mafanikio makubwa ya ongezeko la wajawazito kujifungulia hospitali, bado kuna changamoto ya baadhi yao kuchelewa kufika hospitali na kujikuta wakijifungulia njiani wanapokuja hospitali, jambo ambalo bado linahatarisha maisha ya mama na mtoto.

   "Niwasihi kina mama wajawazito, pindi wanapohisi au kuona viashiria vya kujifungua, wawahi hospitali ili waweze kupata huduma stahiki, kujifungulia nyumbani au njiani ni hatari sana, kunaweza kupoteza maisha ya mama au mtoto ama wote wawili"amesisitiza Dkt. Kinabo

   Jengo hilo la mama na mtoto  limegharimu kiadi cha shilingi milioni 130, ikiwa ni fedha za mapato ya ndani ya halmashauru ya Arusha na lilianza kujengwa rasmi mwaka wa fedha 2018/19 na kukamilika 2019/2020 na kuanza kutumika kwa wamama wajawazito.










Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.