Na Elinipa Lupembe
Kufuatia mpango mkakati wa serikali wa kuboresha miundombinu ya elimu hususani kwenye shule kongwe nchini, wizara ya Elimu kupitia mradi wa EP4R imetoa fedha, kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajli ya ukarabati wa mabweni shule ya sekondari Ilboru, halmashauri ya Arusha.
Akizungumza wakati wa kukagua maendeleo ya mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, amethibitisha mapokezi ya kiasi hicho cha fedha kutoka Serikali kuu, kwa ajili ya ukarabati wa mabweni manne shule ya sekondari Ilboru na tayari utekelezaji wa mradi huo unaendelea na uko katika hatua za mwisho za ukamilishaji.
Aidha ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha, kwa kuwa mabweni ya shule hiyo yalikuwa kwenye hali ya uchakavu uliotokana na kujengwa zaidi ya miaka 50 iliyopita.
"Tumenza mwaka mpya wa fedha 2022/2023 vizuri, mwishoni mwa mwezi Julai tumepokea fedha hizo za ukarabati wa mabweni ya shule yetu kongwe ya Ilboru, ukarabati huu utawezesha wanafunzi kulala kwenye mazingira rafiki". Amefafanua Mkurugenzi Maumi
Naye Mkuu wa Shule ya sekondari Ilboru, Mwl. Denis Otieno, amebainisha kuwa fedha hizo zimekuja wakati muafaka kwa kuwa mabweni hayo yalikuwa yamechaka, ukarabati huu ni wa msingi sana kwa wanafunzi na shule kwa ujumla wake.
"Mabweni yalikuwa yamechoka, yalijengwa mwaka 1963, ukarabati huu, utawezsha watoto kulala kwenye mazingira safi na rafiki, jambo ambalo tunaamini litakuwa na matokeo makubwa kitaaluma katika shule yetu" Amesema Mkuu huyo wa shule.
Aidha amefafanua kuwa, fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 200, zinatumika kukarabati mabweni manne, ikiwemo kubadilisha mapaa, kubadilisha mifumo ya maji safi na maji taka, mfumo wa umeme, kubadilisha milango, madirisha na vioo vya madirisha, kukarabati vyoo, kuziba nyufa pamoja na kupaka rangi ndani na nje ya majengo hayo.
"Tunaishukuru serikali kwa kuwa mabweni yote manne yanalaza jumla ya wanafunzi 760, huku kila bweni likilaza wanafunzi 190, kwa mazingira bora ya kulala ni uhakika wa afya za wanafunzi na taaluma" Amefafanua Mkuu huyo wa shule
Ifahamike kuwa shule ya sekondari Ilboru ni shule ya wavulana na ni miongoni mwa shule kongwe nchini, yenye jumla ya wanafunzi 860, inayofanya vizuri kitaaluma kwa kushika nafasi 10 bora kitaifa kwa matokeo ya mitihani ya Taifa ya kidato cha nne na cha sita.
ARUSHA DC
TUPO KAZINI✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.