Na. Elinipa Lupembe
Serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan inaendelea na utekelezaji wa kuboresha huduma za afya nchini kwa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kwa lengo la kuondoa vifo vya kina mama na watoto wakati wa kujifungua.
Kufuatia mkakati huo Serikali imetoa shilingi milioni 590 kwa ajili ya upanuzi wa zahanati ya Mwandeti kuwa kituo cha Afya, lengo likiwa ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wanachi waishio maeneo ya pembezoni.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Selema Msumi, amebainisha kuwa, kiasi hicho cha fedha kimetumika kujenga jengo la wagonjwa wa nje, jengo pacha la mama na mtoto na upasuaji, jengo la maabara, jengo la mionzi, jengo la kufulia pamoja na nyumba ya watumishi ya kuishi familia tatu (3 in 1).
"Katika fedha hizi, shilingi milioni 500 ni fedha za tozo ya miamala ya simu, na milioni 90 ni fedha za mapambano dhidi UVIKO 19, na tayari nyumba ya watumishi imekamilika na watumishi wameanza kuishi kwenye nyumba hiyo"Amesisistiza Msumi.
Nao wananchi wa Mwandeti wameishukuru serikali ya awamu ya sita, kwa kuwapa fedha za ujenzi wa kituo cha afya, huduma ambazo hapo awali hazikupatikana na kulazimika kutembea umbali mrefu kuzifuata huku wakitumia gharama kubwa za matibabu na usafiri hasa wakati wa usiku
Diwani wa kata ya Mwandeti Mhe. Logolie Lukumay, amesema kuwa, uwepo wa kituo cha afya Mwandeti utasaidia wananchi ambao waliteseka kutafuta huduma za afya kwa gahrama kubwa na wengine kupoteza maisha kwa kukosa huduma.
Mganga Mfawidhi Zahanati ya Mwandeti, Dkt. Aidan Martine amesema kuwa, uwepo wa nyumba za watumishi katika eneo la kazi, utawaongezea ari ya kufanya kazi na weledi katika kutekeleza majukumu yao, ikiwa ni pamoja na utoaji na upatikanaji wa huduma kwa wagonjwa kwa urahisi na kwa haraka wa muda wote wa siku.
"Daktari na wauguzi wanaposihi ndani ya eneo la kazi, inawarahisishia utekelezaji wa majukumu yao ya kazi, kuingia kazini kwa wakati, kutoa huduma kwa haraka hususani huduma za 'emergence' hasa wakati wa usiku, lakini pia inaongeza wigo kwa wagonjwa kupata huduma kwa saa 24" Dkt. Martine
Zahanati ya Mwandeti iko umbali wa zaidi ya Km 47 kutoka makao makuu ya halmashauri, eneo ambalo wananchi wake waliteseka kwa muda mrefu kwa kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya jambo ambalo lilipelekea baadhi ya watu kupoteza maisha kwa kukosa ama kupata huduma kwa kuchelewa.
ARUSHA DC
KaziInaendelea ✍
PICHA ZA MAJENGO KITUO CHA AFYA MWANDETI
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.