Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amekabidhiwa Gari ya Shule ya Sekondari Oldonyosambu, kutoka kwa Wazazi. Mkurugenzi Msumi, amethibitisha kupokea gari la Shule ya Sekondari Oldonyosambu kwa kuwapongeza na kuwashukuru wazazi kwa kuona umuhimu wa kutoa kitendae kazi hicho muhimu kwenye Shule hiyo.
"Gari hili litawezesha kuwasaidia walimu na wanafuzi wanaotembea umbali mrefu pia katika kufauatilia shughuli za kitaaluma pamojan na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Elimu katika Shule yetu"
Aidha amewaomba Walimu kulitunza gari hilo na kutafuta Dereva makini ambaye atakabidhiwa ili kusiwe na mwingiliano wa walimu kutaka kuliendesha.
ameongeza na kusema kuwa Gari litabadilishwa namba na kupewa (SM) Serikali za Mitaa kwa maana limeshakuwa mali ya Serikali ili kuepusha watakaojitokeza na kutaka kuliuza.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.