• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MKURUGEZI OPEC FUND ASHIRIKI NA WANANCHI KUCHIMBA MSINGI WA BWENI LA WAVULANA SHULE YA SEKONDARI OLDONYOWAS

Posted on: March 30th, 2022

Na. Elinipa Lupembe.

Mkurugenzi wa Umoja wa Nchi zinazozalisha Mafuta kwa wingi Duniani (OPEC FUND), Dkt. Alkhalifa Abdulhamid Saleh, ameungana na wananchi wa kijiji cha Oldonyowas, halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, kuchimba msingi wa bweni la wavulana shuke ya sekondari Oldonyowas, mradi unaotekelezwa na TASAF awamu ya IV kwa ufadhuli wa OPEC FUND.

Mkurugenzi huyo wa OPEC FUND, na jopo lake wamejikuta wakishiriki zoezi hilo wakati alipotembelea shuleni hapo, kukagua na kufanya tathmini ya miradi inayofadhiliwa na Umoja huo nchini,  kupitia Mfuko wa Maendelea ya Jamii - TASAF na kukuta kundi kubwa la wananchi wa kijiji hicho, wakichimba msingi wa ujenzi wa bweni la wavulani, ikiwa ni uchangiaji wa asilimia 10 ya nguvu za wananchi katika miradi ya TASAF.

Dkt. Alkhalifa na wenzake  amewiwa kushika zana na kutoa udongo, mara baada ya kukvutiwa na kazi hiyo waliyokuwa wakifanya kwa umoja, ikiwa ni hatua za awali za ujenzi wa mabweni mawili ya wavulana shuleni hapo, mradi unaotekelezwa na TASAF awamu ya IV kwa gharama ya shilingi milioni 338.7, fedha za ufadhili wa OPEC FUND.

"Nimefurahi kuona wanachi tuliowakusudia wanafurahia miradi na kujitoa kuongeza nguvu kazi zao, ili kukamilisha miradi hiyo, inadhihirisha OPEC inashirikiana na Watanzania wenyewe, miradi tuliyoifadhili inafanya kazi iliyokusudia, shule ina miundombinu ya kutosha, watoto wanasoma kwenye mazingira mazuri, wanalala kwenye mabweni mazuri, jengo zuri la utawala na nyumba nzuri za walimu, hii itasaidia kupunguza umaskini kwa jamii" amesisitiza Dkt. Alkhalifa

Licha ya kuridhishwa na utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na OPEC nchini, ameishukuru serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wenye mafanikio makubwa kwa jamii, na kuweka wazi kuwa, Umoja huo utaendelea kushirikiana na serikali, katika kupambana na wimbi la umasikini nchini kwa kuimarisha sekta ya elimu na afya.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Tanzania, Ladislaus Mwamanga, amefafanua kuwa mradi huo mpya wa ujenzi wa bweni la wavulana, unatekelezwa na TASAF awamu ya IV kwa ufadhili wa OPEC FUND na utagharimu kiasi cha shilingi milioni 330.7, bweni ambalo linategemewa kulaza wanafunzi 160.

Mwamanga ameweka wazi kuwa, ugeni huo kutoka OPEC FUND, umekuja kwa ajili ya kufanya mapitio ya kawaida pamoja na kufanya tathimini ya miradi iliyotekelezwa na fedha kutoka OPEC FUND, fedha ambazo walizitoa kama mkopo walipokutana na Mheshimwa Rais, Samia Suluhu Hassan, kiasi cha milioni 50 za Kimarekani, sawa na shilingi bilioni 120, kwa ajili ya kuendeleza mradi wa kupunguza umasikini nchini kwa awamu ya nne, katika mikoa mitano ya Tanzania Bara, ya Arusha, Njombe, Simiyu, Mwanza na Geita.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Oldonyowas, Mhe. Godfray Ayo, amesema kuwa wananchi wa Oldonyowas, wamenufaika sana na miradi inayofadhiliwa na OPEC FUND na kutekelezwa na TASAF, kutoakana na ukweli kwamba, asilinia 90 ya majengo katika shule ya sekodnari Oldonyowas yamejengwa kwa fedha za TASAF.

"Kijiji chetu kimenufaika sana na miradi ya TASAF, ndoa za utotoni zimekoma kwa kuwa watoto wetu wa kike, wamepata fursa ya kusoma kwa kuwa wanalala shuleni, kwenye mabweni yaliyojengwa na TASAF, zamani wasichana hawa wangeolewa, tunaishukuru sana serikali na wafadhili wetu" ameweka wazi Mwenyekiti huyo. 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF imetoa jumla ya shilingi milioni 747.7, kwa ajili ya kutekelza miradi ya kuondoa umaskini katika kijiji cha Oldonyowas, huku shilingi milioni ........ sawa na asilimia .....zikitumika kuimarisha miundombinu ya ahule ya sekondari Oldonyowas.

ARUSHA DC

KaziIendelee✍✍✍




Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • DKT. PASCAL KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 19, 2025
  • WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 18, 2025
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI

    June 17, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.