Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha Dk. Wilson mahera amefanya kikao na watumishi wa Idara ya Afya kwneye Hospitali ya Wilaya ya Olturumet na kukumbushana majukumu yao ya kazi hasa katika kuwahudumia wagonjwa zaidi kufanyakazi kwa kutekeleza mapango mkakati wa halmshauri.
Mkurugenzi huyo amesikiliza kero za watumishi hao na kufanikiwa kutatua palepale zile zinazowezekana na kuahidi kutatua kero zote hasa zile za upungufu wa vifaa pamoja na kuwataka wafenye kazi kwa bidii kwa kuweka uzalendo mbele na kuachana na malalamishi yasiyo ya msingi hasa kwa viongozi wao kwa kuwa kiongozi lazima atumie hata lugha ya ukali pale anapoona kuna uzembe unaosababisha mkwamisho.
Hata hivyo amewataka viongozi na wasimamizi wa atumishi hao kutenda haki kwa watumishi walio chini yao jambo ambalo litaondoa malalamiko yasiyo na msingi yanayoleta chuki katika eneo la kazi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.