Wajumbe wa Baraza la Madiwani wamefanya Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwa wa kuwasilisha taarifa za kata katika ukumbi wa Mikutano Halmashauri ya Arusha.
Katika Mkutano huo waheshimiwa madiwani wamewasilisha taarifa za robo ya tatu kuanzia mwezi Januari -Machi, 2017 za kata 26 ndani ya Halmashauri.
Taarifa hizo zimej umuisha taarifa za mapato na matumizi ya kata husika, taarifa za Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa kwenye kata katika sekta zote Elimu, Afya, Maji, Kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na Mazingira, Taarifa za Kiutawala katika kata, Taarifa za huduma za Jamii, Maafa, Magonjwa nk.
Aidha taarifa hizo zilihusu Miundombinu ya barabara pamoja na Ulinzi na Usalama wa kata, changamoto zinazosababisha mkwamo na mipango mikakati ya kata hizo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.