Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule anawatangazia wananchi wote kuwa tarehe 03.12.2020 kutakuwa na Mkutano wa Baraza la Madiwani, utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, kuanzi saa 03:00 asubuhi.
Mkutano huu ni wa kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika 28. 10.2020, ni mkutano wa kawaida kwa mujibu wa Kanuni na Sheria za Serikali za Mitaa.
Mambo yatakayofanyika kwenye Mkutano huo ni pamoja na Kugawa Vyeti vya Ushindi kwa Madiwani, Madiwani Kuapishwa, Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, Kuunda Kamati za Kudumu za Halmashauri na Uchaguzi wa Wenyeviti wa Kamati hizo.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji atawasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli za Maendeleo za Halmashauri kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai mpaka Novemba 2020, pamoja na kuwasilisha Rasimu ya Ratiba ya Vikao vya Kamati za kudumu na Mikutano ya Halmashauri.
Kamishina wa Maadili atawasilisha Tamko la Viongozi wa Umma kuhusu Rasilimali na Madeni ya viongozi.
NYOTE MNAKARIBISHWA.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.