Madiwani wa kata 27 halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru wamewasilisha taarifa za kata zao kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la kuwasilisha taarifa za kata kwa kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2017/18.
Taarifa zilizowasilishwa ni za miezi mitatu kuanzia mwezi Julai mpaka Septemba, 2017.
Katika mkutano huo Madiwani hupata fursa ya kuwasilish taarifa mbalimbali za kata ikiwemo taarifa za fedha Mapato na Matumizi, taarifa za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ngazi ya kata, taarifa za Elimu, Afya, Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii, Hali ya Chakula katika kata pamoja na taarifa za ulinzi na usalama wa kata.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.