MKUU WA MKOA WA ARUSHA,PAUL MAKONDA AKUTANA NA ASASI ZA KIRAIA NA KUFUNGUA MILANGO YA MASHIRIKIANO KATIKA KUWATUMIKIA WANANCHI.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amekutana na kufanya mazungumzo na Mashirika na Asasi za kiraia zinazofanya kazi Mkoani Arusha kwa lengo la kujenga umoja na mshikamano na ofisi yake na Ofisi yake ili kuongeza kasi ya maendeleo kwa Wananchi.
Mhe. Makonda ameyazungumza hayo mapema leo Julai 08, 2024 wakati wa Mkutano wake na Taasasi zisizo za Kiserikali zinazoshughulika na maendeleo ya huduma za jamii katika Mkoa wa Arusha ikiwa ni mwendelezo wa kazi zake za kukutana na Taasisi na makundi ya watu mbalimbali kwa lengo la kufahamiana, kushirikiana na kuona jitihada wanazozifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo.
"Nitumie fursa hii kuwakaribisha kuitumia ofisi ya Mkoa kama sehemu ya ofisi yenu,Jambo lolote unaloweza kuwa nalo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya mkuu wa wilaya ni ofisi yako.Unapaswa kwenda kifua mbele na kuomba Ofisi hizi ziwasaidie kutatua changamoto zenu ili tu ufanikishe kile unachokifanya ambacho sisi tunaamini ndicho kinachoweza kuleta tija kwenye maisha ya wananchi tunaowaongoza." ameongeza Mhe. Makonda.
Mhe.Makonda amesema Kikao hicho pamoja na mambo mengine kitumike kuzileta Asasi hizo za Kiraia pamoja ili kufanya kazi kwa mashirikiano ya karibu na Serikali katika mkakati wa kuwaletea wananchi maendeleo. Katika Mkutano huo wadau wa Asasi hizo za kijamii wamepata fursa ya kutoa maoni na changamoto zinazozihusu Taasisi zao kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Makonda ambaye ameahidi kuzifanyia kazi katika kuongeza ufanisi na kasi ya utendaji wao wa kazi ili kuweka mazingira rafiki ya Asasi hizo katika kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Arusha
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.