Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda leo Julai 8, 2024 amekutana na kufanya kikao na Maafisa wa TRA ,Mwenyekiti wa Halmshauri ya Arusha,Mkurugenzi wa Halmshauri ya Arusha pamoja na Maafisa Biashara na Ushirika kwa lengo la kubadilisha uzoefu na ushauri wa Kikodi kwa Halmashauri ya Arusha.
Katika Kikao hicho Maafisa toka TRA walitoa ushauri kwa Halmashauri ya Arusha kuhusu mbinu mbalimbali wanazozitumia kukusanya kodi na kufikia malengo waliyopangiwa na Serikali kwa mwaka. Ikumbukwe kuwa moja ya jukumu kubwa la Halmashauri ni pamoja na ukusanyaji maduhuri ya Serikali kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali.
Kwa upande wake Mhe. Kaganda amewapongeza TRA kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji kodi na kuvuka malengo kwa kufikisha asilimia 116 katika Wilaya ya Arumeru kwa kipindi cha Januari - Juni 2024
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.