Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Mhe.Amir Mohammed Mkalipa ameawata Wazazi wote ndani ya Wilaya ya Arumeru kuhakikisha ifikapo tarehe 13/01/2025 watoto wote wanaopaswa kwenda shule wawe wamefanya hivyo kinyume chake watachukuliwa hatua za kisheria.
Hayo ameyazungumza leo tarehe 11/01/2025 katika Kijiji cha Loovilukunyi Kata ya Kisongo katika Halmashauri ya Wilaya Arusha mara baada ya kukagua ukamilishwaji wa majengo ya shule mpya yaSekondari Loovilukunyi na kisha kuzungumza na Wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanika shule hapo.
Mhe,Mkalipa amesema suala la Elimu kwa watoto ni la lazima na Serikali inayoongozwa na Rais Dkt.Samia imeshaweka miundombinu vizuri ili kuwawezesha watoto kupata elimu ya msingi mpaka sekondari bure,na kuongeza kuwa Serikali haitasita kumchukulia hatua mzazi au Kiongozi wa Kijiji,Mtaa au Kata atakayeshindwa kusimamia suala la mtoto kujiunga na masomo kwa kigezo cha kuolewa.
" Niseme tu,hatutamfumbia macho mtu yeyote atakaye leta uzembe wa kutopeleka mtoto shule eti kwa kisingizuo ameshindwa kumpa mahitaji ya sare,daftari na chakula kwani gharama kubwa imebebwa na Serikali" alisema Mhe.Mkalipa.
Katika kuhakikisha suala la wanafunzi waliopangwa wanajisajili kuanza masomo siku ya tarehe 13/01/2025, Mhe.Mkalipa amemwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha Maafisa Elimu na Walimu wanaandaa taarifa ya hali ya kujisajili kwa wanafunzi hao wa shule za awali,msingi na sekondari na kuiwasilisha kwake.
Kwa upande wake,Diwani wa Kata hiyo ya Kisongo Mhe.Godson Lotha Loning'o amemshukuru Mhe.Rais Dkt.Samia kwa kutoa shilingi milioni 584 kwaajili ya ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa,maabara pamoja na matundu ya vyoo ambapo uwepo wa shule hiyo mpya utapunguza umbali ambao watoto waliokuwa wakiutumia kwa siku ili kufuata elimu.
Shule ya sekondari Loovilukunyi ni shule mpya iliyojengwa kwa lengo la kuwapunguzia umbali mrefu watoto wa jamii ya kifugaji waliokuwa wanatumia kutafuta elimu.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.