Waziri Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Boniface Simbachawene akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi wa Arusha DC bwana Seleman Msumi mara baada ya kutembelea banda la maonyesho la Wilaya ya Arumeru kwenye Maonesho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Dodoma.
Mhe. Simbachawene alipata maelezo mafupi kuhusu huduma zinazotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kwa upande wa Utumishi na huduma zinatolewa kwa Wananchi ndani ya Mkoa wa Arusha.
Sambamba na kuzipongeza Halmashauri za Arusha na Meru kwa kazi nzuri za kuwatumikia wananchi pia amezitaka Halmashauri hizo kuendelea kuzifungua barabara za vijijini ili kuongeza kasi ya uwekezaji hususan ujenzi wa Mahotel kutokana na Halmashauri hizo kuwa na vivutio vingi vya Utalii
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.