Na. Elinipa Lupembe.
Mradi wa Binti na Maendeleo unaotekelezwa na Shirika la DSW Tanzania, umefanikiwa kuzui ndoa za utotoni kwa wasichana waliokuwa wamechumbiwa tayari kuolewa, kwa kuwafanya wasichana hao, kukataa kukatisha masomo yao na kuolewa badala yake kuendelea na masomo yao, mrafi unatekelezwa kupitia vikundi vya uelimishaji rika pamoja na klabu za wapinga ukatili ndani ya shule za msingi.
Hayo yamewekwa wazi wakati wa mdahalo, uliohusisha wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya kijamii, wakati wa Bonanza maalum la Binti na Maendeleo, liliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Musa kata ya Musa, halmashauri ya Arusha, Bonanza lenye lengo la kupaza sauti ya kuelimisha jamii juu ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Wakizungumza wakati wa mdahalo huo, kwa pamoja wameupongeza Mradi wa Binti na Maendeleo, mradi ambao wamethibitisha kuleta mapinduzi makubwa kwa kuwajengea uwezo wa kufahamu na kutambua, uhalisia wa suala zima la ukatili wa kijinsia, husani ukeketaji na ndoa za utoto pamoja na madhara yake, ukatili ambao ulikuwa ukifanyika katika maeneo hayo kutokana na mila na desturi za kabila la kimaasai, ambazo wanadai wao wamerithi kutoka kwa wazazi na mababu zao.
"Kupitia elimu inayotolewa na vijana waelimisha rika walio nje ya mfumo rasmi wa elimu, na klabu za watoto shule ya msingi Olchoruvus, jamii yetu ya Musa sasa imepata kufahamu madhara ya ukeketaji na kuanza kuachana na mila hiyo na zaidi jamii imetambua umuhimu wa kuwasomesha watoto wa kike, watoto ambao hapo awali walikatishwa masomo na wazazi wao na kulazimika kuolewa katika umri mdoago" wamesisitiza Wanajamii ya Musa
Hosiana Rafael mwanafunzi wa shule ya msingi Olchorovus, amebainisha kuwa, kupitia klabu yao ya Binti na Maendeleo shuleni, imefanikiwa kuwaelimisha wanafunzi wenzao kupinga na kupambana ukeketaji pamoja na ndoa za utotoni na kuongeza kuwa, elimu hiyo imefanikisha baadhi ya wasichana waliochumbiwa wameweza kuzungumza na wazazi wao na kukata kuolewa na kuamua kuendelea na masomo yao na wazazi wao wamewakubalia.
"Tunashukuru kwa sasa wazazi wetu wameanza kutuelewa, wengi wameanza kutambua madhara ya ukeketaji, na wazazi wengi sasa wameacha kuwaozesha watoto wao wakiwa shule na kuamua kuwaacha waendelee na masomo, na mpaka sasa wasichana hao wapo shuleni, DSW imetuletea ukombozi hasa kwa wasichana wa kata ya Musa" ameweka wazi mwanafunzi Hosiana
Mgeni rasmi katika Bonaza hilo, Afisa Maendelo ya Jamii, Ofisi ya Mkuu wa mkoa Arusha Erena Materu, licha ya kulishukuru shirika la DSW kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa jamii, amewapongeza kwa kuungana na serikali kupambana na ukatili wa kijinsia hususani kwa wanawake na watoto, kazi ambayo ni mkakati wa serikali ya awamu ya sita sambamba na utekeleza wa Ilani ya CCM mbacho ni chama tawala.
Aidha ameipongeza jamii ya watu wa Musa kwa kupokea na kuyatumia maarifa waliyopata na kuwataka kutumia maarifa hayo, kuendelea kuelimishana wao kwa wao, ili jamii nzima ipate uelewa wa pamoja wa kutokomeza mila potofu, mila ambazo zina madhara makubwa kisaikolojia, kijamii na kiuchumi, na kusisitiza kuwa Arusha bila Ukatili inawezekana.
"Haya mambo mazuri tuliyofundishwa na DSW, tuyaendeleze na kuyafanyia kazi kwa kuelemisha wenzetu kwa nguvu moja, tukiungana kwa pamoja kupinga ukatili katika jamii zetu, viongozi wa mila na dini wakisema, viongozi wa serikali na wale vyama vya siasa nao wakisema, baba na mama wakisema, vijana wa kike na wakiume wakisema, watoto wakisema, ninaamini ukeketaji na ndoa za utotoni zitakwisha na kubaki na jamii huru yenye maamuzi sahihi kwa maendeleo ya taifa letu" amesisitiza Elena.
Mratibu wa Mradi wa Binti na Maendeleo shirika la DWS Tanzania, Juliana Mndanga, ameeleza lengo la Bonanza hilo ni kuwakutanisha pamoja, watu wa makundi na mitazamo tofauti, ili kuelemisha na kuwahamasisha kupinga ukatili wa kijinsia kwa sauti moja, kupitia shughuli za kiamii ikiwemo burudani za sanaa za ngoma na nyimbo, michezo, jumbe mbalimbali pamoja na midhalo.
"Kupitia Bonanza hili jamii imeweza kufahamu kuwa jamii yao, inakabiliwa na changamoto ya ukatili wa kijinsia, ukeketaji na ndoa za utotoni, kupitia shughuli mbalimbali zinazofanyika kwenye Bonanza, zinawezesha kutambua madhara ya matukio hayo ya ukatili na namna ya kuyapinga na kuyatokomeza kabisa, huku jamii ikitakiwa kutambua kiwa wakiwapa nafasi wasichana wanawaweza" amesisitiza Juliana.
Hata hivyo Mratibu huyo wa mradi ameweka wazi kuwa, DSW kwa kushirikiana na halmashauri ya Arusha inatekeleza mradi wa Mradi wa Binti na Maendeleo kwenye shule za msingi ndani ya kata tano za Musa, Mwandet, Olmotony, Ng'iresi na Sokon II, huku kukiwa na klabu za kupinga ukatili shuleni na vijana waelimisha rika walio nje ya mfumo rasmiwa elimu.
ARUSHA DC
KaziIendelee✍✍
Mgeni rasmi, Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa masuala ya ukatili wa Kijinsia, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Erena Materu, akizungumza na hadhara ya wananchi wa kata ya Musa,,kwenye Bonanza la Binti na Maendeleo, lililofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Musa na kuratibiwa na shirika la DSW.
Wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya kijamii, wakiwa kwenye Mdahalo wa nini kifanyike kutokomeza Ukatili wa Kijinsia, kwenye kata yao ya Musa, wakati wa Bonanza la Binti na Maendeleo, lililofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Musa na kuratibiwa na shirika la DSW.
Wasichana wa rika tofauti, wakiwa kwenye Bonzanza la Binti na Maendeleo, lililofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Musa na kuratibiwa na shirika la DSW
Wasichana wa shule ya Msingi Musa, wakiwa na bango lenye ujumbe 'Ukatili wa Kijinsia Hamuachi mtu Salama' kwenye Bonzanza la Binti na Maendeleo, lililofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Musa na kuratibiwa na shirika la DSW
Mkurugenzi shirika la DSW, Peter Owaga, akizungumza na hadhara ya wananchi wa kata ya Musa, kwenye Bonanza la Binti na Maendeleo, lililofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Musa na kuratibiwa na shirika la hilo la DSW.
Afisa Mtendaji kata ya Musa, Yustina Mugera akipokea ngao kutoka shirika la DSW, ikiwa ni ishara ya utekelezaji imara wa Mradi wa Binti na Maendleo, unaohusika na kupinga ukatili wa kijinsia hususani ukeketaji na ndoa za utotoni, mradi unaotekelezwa katika kata ya Musa, na tayari matokeo yake yamenaza kuzaa matunda kwa jamii ya wana Musa.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.