Maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya msingi Naisura kijiji cha Lemanda kata ya Oldonyosambu.
Mradi huu unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 306.9,fedha kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Fursa sawa katika Ujifunzaji Bora kwa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST).
Kiasi hicho cha fedha kitajumuisha ujenzi wa jengonla Utawala, vyumba 9 vya madarasa ya , matundu 16 ya vyoo, pamoja na kichomea taka.
Ikumbukwe kuwa, miradi hiyo ya ujenzi wa miundombinu shule za msingi ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, Sura ya tatu Ibara ya 79 kifungu (q)Kukarabati miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na kifungu (C)Kuboresha uratibu na usimamiaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.