Na. Elinipa Lupembe.
Baada ya uzinduzi wa Mradi wa kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika utunzaji bora wa elimu ya awali na msingi Tanzania bara (BOOST) Arusha, timu ya wasimamizi wa mradi huo kitaifa kutoka Wizara ya Elimu, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Bank ya Dunia, hatimaye wamepiga hodi ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, kwa lengo la kujitambulisha na kuanza rasmi utekelezaji wa mradi huo katika halamshauri hiyo.
Katika mazungumzo hayo, timu hiyo ya watalamu, imefafanua kuwa mradi huo wa BOOST unalenga kuimarisha sekta ya elimu ya msingi nchini katika nyanja mbalimbali, kuanzia ngazi ya elimu ya awali, hususani katika maswala ya miundombinu, mpango ambao unatarajiwa kusaidia kuongezeka kwa uwiano wa uandikishwaji wa wanafunzi wa elimu ya awali, pamoja na kuongeza kiwango cha wanafunzi kubaki shuleni
Hata hivyo, Kaim Mkurugenzi halmashauri ya Arusha, mwanasheria Msomi, Monica Mwailolo, baada ya kukamilika kwa mazungumzo na timu hiyo, ameahidi kuwa, halmashauri yake itatekeleza mradi huo kwa weledi na kwa wakati na kuleta matokeo chanya, ili kufikia malengo ya serikali ya awamu ya sita.
Awali, timu hiyo ya watalamu, imefanikiwa kutembea, shule ya msingi Mringa, shule ambayo utekelezaji wa mradi huo umeanza rasmi, katika kipengele cha mafunzo ya walimu.Ikumbukwe kuwa mradi huo wa BOOST, utakoagharimu takriban shilingi Trilioni 1.15, unategemea kutekelezwa nchini kwa kipindi cha miaka mitano na umezinduliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍
Jiandae Kuhesabiwa
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.