Na. Elinipa Lupembe.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi, Saad Mtambule leo amemkabidhi fomu za Uteuzi wa Ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi, Bw. Ramadhani Lila Msoma kupitia chama cha Alliance to Africa Farmers Part -AAFP,
Mgombea huyo aliwasili kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo, eneo la Sekei akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, majira ya saa 06:00 mchana, na kukabidhiwa fomu hizo za Uteuzi mnamo saa 06:17 mchana, akiwa ni mteule wa chama cha AAFP kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo.
Aidha Msimamizi huyo wa Uchaguzi, amemkabidhi fomu ya Uteuzi mgombea huyo, kufuatia Maelekezo ya Fomu ya Uteuzi Na. 8B, kwa mujibu wa Kifungu cha 38 (3) na (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 ikiweka wazi mambo yaliyojumuishwa kwenye fomu ya Uteuzi.
Hata hivyo Mtambule, amemtaka mteule huyo, kuchukua muda kusoma melekezo yanayotolelewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kupitia vitini vya maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, sambamba na kuheshimu taratibu za uchaguzi kwa kufuata maelekezo hayo kutafanya uchaguzi kuwa wa amani, huru na haki kwa manufaa ya watanzania wote.
Mgombea huyo amefanya kufikisha idadi ya Wagombe saba kutoka vyama saba vya siasa, kuchukua fomu ya Uteuzi wa Ubunge kwa Jimbo la Arumeru Magharibi.
PICHA ZA MATUKIO
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbonla Arumeru Magharibi Saad Mtambule (kulia), akimkabidhi fomu ya Uteuzi wa Mbunge Jimbo la Arumeru Magharibi kupitia Chama Alliance to African Farmers Part - AAFP, Bw. Ramadhan Lila Msoma.
Bw. Ramadhani Lila Msoma wa chama ca AAFP, akisani kitabu cha kukiri kipokea fomu ya Uteuzi wa Ubunge, mara baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.