Jumla ya Wanafunzi 6,506 wa kidato cha pili katika shule 49 za sekondari halmashauri ya Arusha wameanza leo mitihani ya taifa mwaka 2017.
Afisa Vifaa na Takwimu Halmashauri ya Arusha mwalimu Philip Mwakapalila amefafanua kuwa kati ya wanafunzi hao wasichana ni 3,489 na wavulana ni 3017 na jumla ya masomo 14 yatafanyiwa mitihani hiyo.
Ameongeza kuwa kati ya masomo kumi na nne, masomo 12 ni ya lazima kufanywa na wanafunzi wote na masomo mawili ni ya kuchagua yaani 'option' ambayo ni masomo ya Biashara yaani Book Keeping na Commerce.
Mwakapalila amesema kuwa wanafunzi hao wameandaliwa vizuri kiakili na kisaikolojia hivyo wanategemea kupata matokeo mazuri ya ufaulu katika mitihani hiyo.
Uongozi wa halmashauri ya Arusha unawatakia kila la kheri katika mitihani yao waweze kufaulu na kuendelea na kidato cha tatu na hatimaye kutimiza ndoto zao za matarajio yao.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.