• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mwarobaini wa madini ya Floraidi Lemanda wapatikana

Posted on: August 24th, 2018

Kufuatia mikakati ya Serikali ya awamu ya tano, ya kujikita zaidi katika kupambana na  kutatua changamoto sugu zinazowakabili wananchi wake, Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji, imetoa mtambo maalumu wa kuondoa kiwango cha madini ya Floraidi yaliyozidi  kwenye maji ya kunywa yanayoyatumia na wananchi wa kijiji cha Lemanda kata ya Oldonyosambu, halmashauri ya Arusha.

Mtambo huo umewashwa rasmi kwa majaribio,  mara baada ya watalamu wa kampuni ya O2andB kuusimika kwenye eneo la shule ya msingi Oldonyosambu, tayari kwa kuanza kuchuja maji ili kupunguza kiwango cha madini ya Floraidi yaliyozidi kwenye maji.

Akizungumza wakati wa kusimika mtambo huo, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, amethibitisha kupokea mtambo huo kutoka serikali kuu, mtambo unaojulikana kwa jina la CDI 'Capacity of Dionization system, mtambo uliotengenezwa na Kampuni ya O2andB ya chini Korea.

Amefafanua kuwa mtambo huo una uwezo wa kupunguza kiwango cha madini ya Floraidi yaliyozidi pamoja na chumvi kwanye maji,  kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kuchuja maji bila kutumia kemikali.

Hata hivyo Dk. Mahera amekiri kuwa, mtambo huo una uwezo wa kuchuja maji na kupunguza kiwango cha Floraidi kutoka miligram 18.7 kwa lita moja hadi kufikia miligram 0.37 kwa lita moja, na kuongeza kuwa ni dhahiri kuwa tatizo hilo linakwenda kwisha na kuleta matumaini mapya kwa wananchi wa Lemanda, wananchi ambao wamepata athari kubwa za kimwili na  kisaikolojia kufuatia madhara yatokanayo na kunywa maji yenye madini ya Floraidi iliyozidi kwa miaka mingi.

" Madhara yatokanayo na Floraidi sasa yamefikia mwisho kwa wakazi wa Lemanda, tunategemea sasa wananchi kutumia maji safi na salama yasiyo na Floraidi kama ilivyokua hapi awali" amesema Mkurugenzi Mahera

Naye Diwani wa kata ya Oldonyosambu Mheshimiwa Raymond Lairumbe, ameipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Magufuli kwa kusikia kilio cha wananchi wa Lemanda,  ambao kimsingi wengi wao wamepata madhara makubwa sana kutokana na kutumia maji yenye kiwango kikubwa cha madini ya Floraidi huku watoto  wakiathirika zaidi mifupa ya miili yao kwa kupinda miguu na kuwa na vichwa vikubwa.

" Nichukue fursa hii kumpongeza mheshimiwa Rais, Doctor John Pombe Magufuli, kwa kuwaonea huruma wananchi wa Lemanda, na serikali ya awamu ya tano kwa ujumla, serikali inayowajali wananchi bila kubagua itikadi zao, leo Lemanda tumepata mtambo wa kuondoa Floraidi kwenye maji " amesema Diwani huyo.

Aidha amewataka wananchi wote wa kijiji cha Lemanda, kuhakikisha wanafika shuleni hapo kuchota maji kwa ajili ya matumizi ya kupikia na kunywa, kwa kuwa madhara ya Floraidi yanatokana na kula chakula kilichopikiwa maji yenye madini hayo pamoja na kunywa maji.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Lemanda,  Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Lemanda, Gaspa Mollel amesema kuwa, mtambo huo ni muhimu na neema kwa  wananchi wa eneo hilo kutokana na ukweli kwamba, wananchi walikuwa wamekata tamaa ya kupata maji safi na salama, huku akiahidi kuongoza wananchi hao kuutunza mtambo huo, pamoja na kuendelea kuwahamasisha wananchi, juu ya umuhimu wa wananchi hao kutumia maji hayo safi na salama.

Naye Msimamizi Mkuu, Maabara ya Ubora wa maji mkoa wa Arusha, Jovitus Kichumu amesema kuwa, kiwango cha madini ya Floraidi kwenye maji yanayopatikana Lemanda ni miligramu 18.7 kwa lita moja, kiwango ambacho ni kikubwa sana na kisichofaa kwa matumizi ya binadamu na kufafanua kuwa mtambo huo unauwezo wa kuchuja na kupunguza mpaka kufikia kiasi cha miligram 0.37 kwa lita kiwango ambacho kinakubalika kimataifa.

Aidha Mhandisi wa Mitambo wa Kampuni ya O2&B Derick Erastus, amesema mtambo huo unauwezo wa kuchuja lita 20,000 za maji kwa siku na unatumia umeme mdogo wa Volti  1.5V na unauwezo wa kudumu miaka mitano mpaka saba bila kufanyiwa matengenezo.

PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KUSIMIKA MTAMBO HUO.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari Oldonyosambu juu ya umuhumi wa mtambo huo.

Diwani wa kata ya Oldonyosambu mheshimiwa Raymond Rairumbe akizungumza na wakazi wa Lemanda wakati wa kusimika mtambo wa kuondoa madini ya Floraid kwenye maji.


Wanafunzi wa shule ya Msingi Oldonyosambu wakichota maji yaliyochujwa na kuondolewa madini ya Floraidi mara baada ya mtambo kuwashwa.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.