NA Elinipa Lupembe.
Halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, imejipanga kuhakikisha kuwa wafanyabiaashara wakubwa hawachukui vitambulisho vya machinga bali wanalipa kodi stahili kulingana na aina na mitaji ya biashara zao, kwa elimu kwa wafanyabiashara juu umuhimu wa kulipa kodi.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mheshimiwa Ojung'u Salekwa wakati wakiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwakwe kuhusiana na mikakati ya namna gani watakukusanya mapato ya halmashauri na kuweza kufikia malengo waliojiwekea bila kuathiri vitambulisho vya wajasiriamali wadogo.
Amefafanua kuwa, kumekuwepo na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kudanganya na kuchukuwa vitambulisho vya machinga ili kukwepa kukadiriwa kodi inayostaili, hali inayosababisha halmashauri hiyo kusuasua kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato kwa robo ya kwanza ya bajeti ya mwaka 2020/2021.
Mwenyekiti huyo, ameeleza kuwa, halmashauri imejipanga kutumia watalam wa ndani kutembelea biashara na kubaini maeneo ya wafanyabiashara wakubwa ili kutoa elimu na kuwakadiria mapato yanayostaili na kuwathibiti wasiweze kuchukuwa vitambulisho vya machinga litakapoanza zoezi za ugawaji wa vitambulisho hivyo.
"Tunashirikiana na Mkurugenzi pamoja na wataalam wetu kuwaelewesha na kuwaelimisha umuhimu wa kulipa kodi kwani wanapolipa kodi ni kwafaida yao ,kwani kodi hizo ndizo zinazotumika kuleta Maendeleo ya nchi ikiwemo kujengea barabara na vituo vya afya pamoja na huduma zingine za kijamii" alibainisha Mwenyekiti Ojung'u
Aliongeza kuwa wanasubiri vitambulisho vipya vya machinga vilivyoboreshwa na kuhakikisha kuwa watakao pewa ni wamachinga halisi na sio wafanyabiashara wanaokwepa kodi na kusababisha halmashauri kushindwa kufikia malengo yake
Aidha alifafanua kuwa mapato ndio roho ya halmashauri ambapo kuna maeneo ikiwemo eneo la uchimbaji wa mchanga la Osunyai,wamewaondoa baadhi ya mawakala na kuwaweka wanajeshi wa JKT Suma jambo ambalo limeshaonyesha matokeo chanya.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mheshimiwa Ojung'u Salekwa, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Madiwani, wakati wa mkutano wa robo ya pili mwaka wa fedha 2020/2021, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halamshauri hiyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.