• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MWENYEKITI HALMASHAURI YA ARUSHA, AITAKA JAMII KUHAKIKISHA WAJAWAZITO NA WATOTO WANAHUDHURIA KLINIKI

Posted on: April 6th, 2022

Na. Elinipa J. Lupembe.

Jamii imetakiwa kuwahudumia kina mama wajawazito na watoto kwa kuhakikisha wanahudhuria kliniki kipindi chote cha ujauzito, sambamba na kuwapatia lishe bora, huku wakisisitizwa wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na sio nyumbani.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti halmasahuri ya Arusha, na Diwani wa Kata ya Laroi, Mhe. Ojung'u Salekwa, alipotembelea zahanati ya Imbibya kata ya Mwandeti, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na hali ya upatikanaji wa huduma za afya katika vituo vya afya vya halmashauri hiyo.

Mwenyekiti Ojung'u licha ya kuridhishwa na upatikanaji wa huduma za afya katika vituo vya afya vya serikali katika halmasahuri hiyo, lakini pia amebaini changamoto za baadhi ya kinamama wajawazito kutokuhudhuri kliniki, wengine kujifungulia nyumbani, kutokuzingatia lishe bora kwa siku 1000 za ujauzito huku baadhi ya kinamama kuacha kuwapekeka kliniki watoto wa kabla ya kutimiza umri wa miaka mitano.

"Tunapaswa kutambua kuwa, suala la ujauzito ni la familia na jamii nzima, hivyo ni vema wote kuzingatia kumlea mjazito kwa kuhakikisha anahudhuria Kliniki mara anapohisi ana ujauzito, kumpa lishe bora kwa siku 1000 za ujauzito pamoja na kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na si nyumbani, na baadaye kiwapeleka watoto kliniki mpaka watakapofikisha umri wa miaka mitano" amesisitiza Mwenyekiti Ojong'u

Aidha Mwenyekiti Ojung'u amesisitiza kuwa serikali inaendelea kutekeleza mkakati wa kufikisha huduma za afya karibu na wananchi na zaidi imewekeza nguvu nyingi katika kuboresha miundombinu ya afya na kuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeimarika, hivyo amewasisitiza wananchi  kutumia huduam hizo kwa kuwa zinapatikana katika maeneo yao sasa.

Naye mama Yohana, mama aliyemleta mtoto wake kliniki, zahanati ya Imbibya, amesema kiwa kwa sasa jamii yao ya kimaasai imepata uelewa mkubwa wa kuhudhuria kliniki na kujifungulia hospitali jambo ambalo hapo awali halikiwepo kabisa.

"Kwa sasa kinamama wengi tunajifungulia hospitali, zahanati yetu ya Imbibya inatoa huduma zote za afya ya uzazi, tunapewa ushauri wa masuala ya lishe, kujikinga na magonjwa, niwashauri kina mama wajawazito wote wa Mwandeti, kuhudhuria kliniki, kujifungulia hospitali pamoja na kuwapeleka watoto klini mpaka watakapofikia miaka mitano, jambo ambalo linahakikishia afya ya mama na mtoto" amesisitiza mama Yohana.

Hata hivyo Mratibu wa Afya ya Uzazi, Muuguzi Bujiku Butolwa amewasisitiza wajawazito kuhudhuria klini na wenza wao, ili wote kwa pamoja wafahamu maendeleo ya afya ya mama na mtoto aliyeko tumboni, pamoja na kupata elimu na ushauri wa utunzaji na ukuaji wa mimba.

Pia mtatibu huyo, amefafanua  umuhimu wa mama mjamzito kuhudhuria kliniki kwa wakati ni pamoja na kupata dawa muhimu za kuongeza damu, kuzuia minyoo na malaria, kupima vipimo muhimu, kama uuna tatizo litatuliwe mapema,  vipimo hivyo Ni wingi na group la damu, kupata elimu ya Lishe wakati wote wa ujauzito.

"Ni jukumu la familia kumuwezesha mama mjamzito kuhudhuria kliniki kipindi chote cha ujauzito, kumuwahisha kituo cha afya pindi anapohisi uchungu wa kujifungua, ni hatari mjazito kujifungulia nyumbani anaweza kupoteza maisha yake na mtoto, ni vema familia nzima kumtunza na kumsaidia mama mjamzito kujifungulia hosoitali" Amesisitiza Mratibu huyo wa Afya ya Uzazi.

Halmashauri ya Arusha ina jumla ya hospitali 2, vituo 7 vya afya na zahanati 49, huku kukiwa na huduma za mkoba 'mobile clinic', vituo hivyo vyote vinatoa huduma zote za afya na uzazi, kwa kina mama wajawazito na watoto.


ARUSHA DC

KaziInaendelea✍✍✍


Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa akiwa watoto waalioletwa Kliniki kwenye zahanati ya Imbibya kata ya Mwandet, kuonyesha hali ya upatikanaji huduma za afya kwenye ameneo ya vijijini.


Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa akiwa amemmbeba mtoto Yohana, aliyeletwa Kliniki kwenye zahanati ya Imbibya kata ya Mwandet.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.