Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha mheshimiwa Noah Lembris amewataka wataalam wa ngazi za vijiji na kata kutumia muda zaidi kujifunza matumizi ya 'Force Akaunti' katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayopelekwa kwenye maeneo yao.
Mheshimiwa Noah amesema hayo alipoongoza jopo la Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekeleza katika mwaka wa fedha 2017/2018, ziara inayofanyika kila robo ya mwaka wa fedha.
Mwenyekiti huyo amesisitiza hayo baada ya kugundua kuwa bado kuna baadhi ya viongozi wa vijiji na kata wanakabiliwa na changamoto ya namna ya kufuata utaratibu halisi wa matumizi ya fedha za miradi zinazopelekwa katika maeneo yao na kuwa na mkanganyiko wa nini hasa kifanyike kutekeza miradi hiyo kwa kutumia forced akaunti.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.