Na Elinipa Lupembe
Mwenyekiti halmashauri ya Arusha, Mheshimiwa Ojung'u Salekwa, amefungua mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Mwenyekiti Ojun'gu amewashukuru wajumbe wote kwa kuhudhuria mkutano na kuwataka kujadili agenda na hoja zote kwa umuhimu wake kwa kuzingatia maslahi mapana ya halmashauri yetu ya kuwahudumia wananchi.
Tuanenda kujadili taarifa ya Mapato na matumizi, pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, huku halmashauri ikiwa imepokea fedha nyingi za miradi ya maendeleo kutoka Serikali Kuu.
"Waheshimiwa Madiwani, tunapojadili hoja na agenda za mkutano, tunatakiwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za vikao vya kisheria kwa kuzingatia zaidi mustakabali wa halmashauri yetu".Amesisitiza Mhe. Ojung'u.
ARUSHA DC
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.