Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii-CHF ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu pindi wanapougua.
Ametoa rai hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utoaji wa huduma za afya pamoja na kukagua ujenzi wa miundombinu ya Kituo cha Afya Nduruma na kuzungumza na wanchi na watumishi wa kituo hicho cha Afya.
Naibu Waziri huyo amesema kuwa serikali imeanzisha mfuko wa Afya ya jamii 'CHF' na tayari imeweka mikakati thabiti ya kuhakikisha wanachama wote wa mfuko huo wanapata matibabu na dawa zote muhimu bila usumbufu wowote na katika vituo vyote vya afya.
Ameongeza kuwa serikali pia inaandaa utaratibu ambao itakuwa ni lazima wananchi wote kujiunga na bima za afya na si hiari tena kama ilivyokuwa hapo awali hivyo wananchi wanapaswa kuanza kuzoea kujiunga na mfuko hiyo sasa.
Hata hivyo Naibu Waziri huyo ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya kituo hicho na kusema kuwa amejihakikishia ubora wa majengo kwa kulinganisha na thamani ya fedha zilizotumika.
Amefafanua kuwa matumizi ya force account' yameonyesha mafanikio makubwa ukilinganisha na kutumia Mkandarasi na kuwataka wananchi Kamati ya Ujenzi kuendelea kushiriki na kufuatilia hatua zote za ujenzi na manunuzi ya vifaa vyote kwa kuwa fedha hizo ni zao.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.