NATAKIWA KUFANYA NINI WAKATI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022.
Unachotakiwa kufanya ni kumpa ushirikiano wa kutosha Karani wa Sensa atakapokutembelea katika kaya kwa kujibu maswali yote atakayokuuliza kwa usahihi.
Aidha, ukiulizwa swali na hujalielewa au hujasikia vizuri, unayo haki ya kumuomba Karani arudie kuuliza au kutoa ufafanuzi ili uweze kutoa jibu sahihi kulingana na swali lilioulizwa.
Ni muhimu kwa Mkuu wa Kaya kuhakikisha anachukua taarifa zote muhimu (kama umri, elimu, jinsi, hali ya ndoa, umiliki wa vitambulisho vya taifa, shughuli za kiuchumi) za watu wote waliolala katika Kaya yeke usiku wa kuamkia siku ya Sensa ili aweze kukumbuka wakati Karani atakapotembelea katika Kaya.
SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022
JIANDAE KUHESABIWA 23.08.2022
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.