• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

BAADA YA CHANGAMOTO YA MUDA MREFU, WANANCHI WA KIJIJI CHA SAMARIA WAPATA NEEMA YA MAJI SAFI NA SALAMA

Posted on: November 19th, 2022

Na  Mwandishi Wetu


Baada ya mateso ya muda mrefu ya changamoto ya upagikanaji wa maji, hatimaye wananchi wa kijiji cha Samaria kata ya Nduruma, Halmashauri ya Arusha, wamepata neema ya kupata maji safi na salama, baada ya serikali kutoa milioni 30 za kukamilika kwa mradi huo wa maji.

Wananchi hao waishukuru serikali kwa kusadia kutekeleza mradi wa maji ya kisima, ambao tayari umeanza kuwanufaisha wananchi hao na kusahau tabu waliyoipata kwa kipindi kirefu, kwa kutumia muda mrefu kutafuta maji, hali iliyosababisha kuzorota kwa baadhi ya shughuli nyingine za kijamii na kiuchumi.

Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, wananchi wamekiri, kukamilika kwa mradi kumekuwa na faida kubwa kwa kuwa, umeondoa adha iliyokuwepo hapo hususani kwa kina mama ambao waliteseka kutafuta maji.

“Sasa tumefikia ukomo wa mateso ya  kutafuta maji,  wanawake wa Samaria, tunaishukuru Serikali kwa kutushika mkono na kukamilisha  mradi, upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama hasa umetuondolea kero kubwa kinama, tunaamini Serikali itaendelea kutusaidia ili maji yafike katika maeneo yote ya kijiji cha Samaria”. Alisema Damari Nnko Mkazi wa Samaria.


Hata hivyo, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Mhe. Noah Lembris, ameweka wazi kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma za muhimu ikiwemo maji safi na salama ndani ya mita 400 huku akiwataka viongozi wa maeneo hayo kusimamia kwa uadilifu mradi huo ili kila mwananchi aweze kunufaika.

“Tunajipanga vyema namna ya kupanua na kuendeleza mradi huu kwa kusogeza huduma ya maji karibu na wananchi, niwaombe wananchi wa tuendelee kuwa wazalendo kwa mradi huu ili uweze kudumu kwa muda mrefu,  shirikianeni na viongozi wa Serikali ya kijiji kuhakikisha mradi unawanufaisha wananchi wote”. Alisisitiza Mhe. Noah

Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, ameishukuru familia iliyotoa eneo kwaajili ya kutekeleza mradi huo na kusisitiza kuwa kila mwananchi ana wajibu wa kutunza miundombinu iliyojengwa katika eneo hilo ili iendelee kuwasaidia wananduruma pamoja na vizazi vijavyo.

“Kwa kipindi kirefu kulikuwa na shida ya maji katika eneo hili, mama zetu walikuwa wanahangaika huku na kule kutafuta maji, mateso yalikuwa makubwa sana, lakini leo tunamshukuru Mungu kwa kukamilika kwa mradi huu, nawasihi kuendelea kutunza miundombinu hii ili iidumu na kuwahudumia wananchi wote”. Amesema Mkurugenzi Msumi.

Aidha Diwani Kata ya Nduruma Mhe. Raymond Mollel, amesema kutokana na historia ya eneo hilo ilisemekana kuwa hakuna uwezekano wa kupata maji katika Kijiji hicho, hivyo uwepo wa kisima hicho ni neema kubwa kwa wakazi wa Samaria.

Mradi wa kisima cha maji ulianza kutekelezwa kwa nguvu za wananchi baadaye Halmashauri ilitoa kiasi cha Milioni 30 fedha za mapato ya ndani na kukamilisha mradi huo.

ARUSHA DC

TUPO KAZINI✍✍


PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA UZINDUZI WA MRADI WA MAJI KITONGOJI CHA SAMARIA








Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.